Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,168
- 39,118
ANAANDIKA MHE.ALFRED SOTOKA MWENYEKITI WA CHADEMA MKOA WA RUKWA.
JESHI LA POLISI LATUMIWA NA DC LIJUALIKALI KUFANYA UNYAMA NA UKATILI WA KUTISHA. WATOTO WACHANGA WAACHWA MAJUMBANI, VIPIGO NA MATESO VYATAWALA WENGINE HAWAJULIKANI WALIPO HADI SASA.
NTALAMILA
Uchaguzi wa serikali za mitaa wa kuwapata Mwenyekiti wa Kijiji, wenyeviti wa vitongoji na wajumbe ulirudiwa tarehe 30/11/2024 katika Kijiji cha NTALAMILA kilichopo Jimbo la Nkasi Kusini na mkoa wa Rukwa. Yaliyojiri katika siku hiyo ya uchaguzi ni kwamba katika vitongoji 10, Wagombea Kupitia CHADEMA walipata vitongoji 5 na wale wa CCM wakapata vitongoji 5 . kwa nafasi ya Mwenyekiti wa Kijiji Chadema ilipata kura 966 dhidi ya Mgombea wa CCM aliyepata kura 634 katika kituo cha Majumuisho. Hata hivyo hakuna aliyetangazwa kuwa mshindi kwa nafasi zote na badala yake MKUU HUYO WA WILAYA YA NKASI PETER AMBROSE LIJUALIKALI aliamrisha wasimamizi na Polisi wakabeba ma-boxi ya kura zote za majumuisho na kuondoka nayo kwenda Namanyere( makao makuu ya Wilaya ya Nkasi). Na bila wasimamizi kumtangaza yeyote Kati ya wagombea hao kuwa ni mshindi.
JANA tarehe 19 -12-2024 DC PETER AMBROSE LIJUAKALI akiambatana na magari mawili yaliyosheheni Askari Polisi, alifika Kijijini hapo Ntalamila ambapo alitisha mkutano wa HADHARA na lengo likiwa ni yeye kuchukua jukumu la Kumtangaza Mshindi wa vitongoji na Mwenyekiti wa Kijiji cha NTALAMILA, huku akiwa sambamba na aliyekuwa Mgombea wa CCM. LIJUAKALI aliwaeleza wananchi waliokuwa wamehudhuria mkutano huo wa hadhara kwamba "Watake wasitake Mgombea wa CCM ndiye Mwenyekiti wa kijiji cha Ntalamila kuanzia leo(yaani jana). Baada ya kauli yake hiyo Wananchi walihamaki na ndipo vurugu zilianza na mkutano huo ukasambaratika.
UOVU NA UKATILI . Usiku wa kuamkia leo tarehe 20-12-2024 Jeshi la Polisi kutoka Wilaya ya Nkasi wakiungana na Askari kutoka Mkoani Rukwa kwa AMRI YA DC LIJUAKALI Walianza kuvamia makazi ya wanachama wa CHADEMA kwa kuvunja nyumba zao (Milango na Madirisha) usiku wa manane na katika kufanya unyama huo polisi wamefanya msako na kuiba fedha na vitu vya thamani na Kuondoka navyo usiku huo sambamba na watu waliokamatwa na Polisi.
Hadi sasa hivi taarifa zinasema Wakina mama zaidi ya 16 wakiwa na watoto wa wachanga walichukuliwa na Askari Polisi na wanaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi Mjini Sumbawanga.
Aidha, jambo la kusikitisha wengi wao wa Mama hao wako katika nguo za kulalia(night dress) na watoto wao wachanga.
Taarifa zilizopo kijiji cha Ntaramila ambapo DC Lijualikali anaongoza unyama huo ni kwamba operation za kuvunja nyumba na kukamata wananchi hadi mashambani wanaodhaniwa kuwa wanachama wa Chadema zoezi linaendelea .
Hali ni mbaya na hakuna mtu anaruhusiwa kujua hali za watu wanaishikiliwa na jeshi la polisi kujua hali zao wanaokadiliwa kufikia sasa idadi ya watu 50 waliokamatwa na wengine hawajulikani walikopelekwa.
Ni muhimu kupazia sauti hili jambo. Wanaharakati wa Haki za Binadamu mtusaidie kupaza sauti.