Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Wakili wa kujitegemea, Peter Madeleka, ameshangazwa na majaji kulalamika mbele ya Rais kuhusu usalama wao, akisisitiza kuwa kisheria, vyombo vya ulinzi na usalama ni vyombo vya Dola na si mali ya Rais au Serikali pekee.
Akizungumza na Jambo TV leo, Januari 14, 2026, Madeleka amefafanua kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaundwa na mihimili mitatu ambayo ni Serikali, Bunge, na Mahakama. Amesema vyombo vya ulinzi kama Polisi vinapaswa kuwajibika kwa mihimili yote mitatu kwa usawa, kwani vinatekeleza amri za kidola bila kuhitaji ruhusa kutoka kwa mhimili mmoja kwenda mwingine.
Wakili Madeleka ameongeza kuwa Jaji Mkuu anayo mamlaka ya kisheria ya kuviamuru vyombo vya dola kutekeleza majukumu ya ulinzi au kuleta watu mahakamani bila kumuomba Rais ruhusa.
Kuhusu suala la rasilimali, Madeleka amehoji kwanini Mahakama iendelee kuomba bajeti au vitendea kazi wakati kila mhimili unapaswa kuwa na fungu lake lililotengwa kisheria ili kuleta ustawi. Amelinganisha hali hiyo na mhimili wa Serikali, ambao hauhitaji kuomba magari au ulinzi kwa mhimili mwingine, bali unatumia mamlaka yake ya kidola.