Peter Madeleka: Mwili wa kijana Enock Elias umekutwa umezikwa kinyemela baada ya kukamatwa na uhamiaji Wilayani Kibondo

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1,242
Reaction score
4,813
Kuna taarifa kuwa mwili wa kijana ENOCK ELIAS SEBAKWIYE umekutwa umezikwa kinyemela baada ya kukamatwa na uhamiaji wilayani KIBONDO tarehe 27 Oktoba 2023 akidaiwa kuwa ni Mkimbizi.

Kama taarifa hii ni kweli, ninalaani kitendo hiki na Wahusika akiwemo Makakala, wawajibishwe.

IMG_9044.jpeg
 
Hii Nchi kungekuwa na Taasisi Fulani huru yenye kufanya upepelezi wa matukio mapovu ya majeshi yetu, nadhani jela zingejaa hawa Jamaa, wakiwa na zile uniform wanajiona katika dunia nyingin kabisa......Pumzika kwa Amani Champ.

Kuna mtu huzi ameandika hii idea. wenzetu wa internal investigation bureau ambayo wao wana deal na makosa ya polisi na ku keep taasis in chek na taasis nyingine ndani ya doj japo si zote.
Huku ni kama hamna limit, wako kwenye free roaming mode na hakuna wa kuwawajinisha kwa namna yoyote
 
Kuna taarifa kuwa mwili wa kijana ENOCK ELIAS SEBAKWIYE umekutwa umezikwa kinyemela baada ya kukamatwa na uhamiaji wilayani KIBONDO tarehe 27 Oktoba 2023 akidaiwa kuwa ni Mkimbizi.

Kama taarifa hii ni kweli, ninalaani kitendo hiki na Wahusika akiwemo Makakala, wawajibishwe.

View attachment 2811202
Huyu dogo na mfahamu sana ..!Ni mtoto wa Mwalimu mstaafu Elias Simbakwiye.Kaka yake ni Afisa Kilimo Tanga Aiseeeee!
 
walikuwa wanajaribu kumu arrest akafa kwenye purukushani ama walim shuti tu barabarani ?

alikuwa mahabusu akafa njaa au natural death ?

alikuwa raia asiye na hatia ama kachero wa Kagame ?

amezikwa kinyemela maana yake nini, kazikwa na nani ? wamekuta maiti shambani ?

ana makaratasi au hana ?
Huyu ni Mtanzania kabisa .Baba yake mzazi alishawahi kuwa Katibu wa CCM wilaya ya Kibondo
 
Kuna taarifa kuwa mwili wa kijana ENOCK ELIAS SEBAKWIYE umekutwa umezikwa kinyemela baada ya kukamatwa na uhamiaji wilayani KIBONDO tarehe 27 Oktoba 2023 akidaiwa kuwa ni Mkimbizi.

Kama taarifa hii ni kweli, ninalaani kitendo hiki na Wahusika akiwemo Makakala, wawajibishwe.

View attachment 2811202
Sasa Madeleka unatetea na wakimbizi? Mtu amekuja nchini kwa njia haramu, huoni kifo chake kuwa ni ahueni kwa Taifa?
 
Kigoma irudishwe Burundi

Ova
Kigoma haikuwahi kuwa sehemu ya Burundi, Kigoma ilipaswa kuwa nchi kamili kama ilivyo Rwanda na Burundi. Kigoma Ina eneo lake linalotambulika, Ina watu ambao ni waha wenye mila zao na tamaduni zao zinazotofautiana kidogo sana na Rwanda na Burundi.

Kigoma ni moja ya mikoa au majimbo yaliyoshirikishwa kikamilifu kuunda Jamuhuri ya Tanganyika. Kukubali kwa Kigoma kuachana na Utawala wake wa kichifu "Mwami" na kukubaliana na Nyerere kuunda Tanganyika na kuuzika ukabila ndio ulioiponza Kigoma ambayo hadi leo watu wake wanatengwa na kubaguliwa ndani ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Watu wasiojua historia ya taifa hili ndio wanaoeneza propaganda za kipuuzi kuwa Kigoma irudi Burundi, kwa bahati mbaya sana watu wa aina hiyo ndio walioajiriwa Serikalini "Uhamiaji" na wanaendeleza ubaguzi unaoweza kuligawa taifa.

Inashangaza sana, Rais wetu ana unasaba na waarabu lakini hakuna anaepaaza sauti kuhoji uhalali wake kuwa Rais, lakini muha wa Kigoma kuonekana kwenye eneo lake ndani ya Afrika ni kosa linalostahili kifo ? Hii dhambi ya kubaguana ndani ya JMT itakuja kupata majibu siku za usoni kama haya yanayotokea sasa kule Gaza, kati ya waisrael na wapalestina.
 
Kigoma haikuwahi kuwa sehemu ya Burundi, Kigoma ilipaswa kuwa nchi kamili kama ilivyo Rwanda na Burundi. Kigoma Ina eneo lake linalotambulika, Ina watu ambao ni waha wenye mila zao na tamaduni zao zinazotofautiana kidogo sana na Rwanda na Burundi.

Kigoma ni moja ya mikoa au majimbo yaliyoshirikishwa kikamilifu kuunda Jamuhuri ya Tanganyika. Kukubali kwa Kigoma kuachana na Utawala wake wa kichifu "Mwami" na kukubaliana na Nyerere kuunda Tanganyika na kuuzika ukabila ndio ulioiponza Kigoma ambayo hadi leo watu wake wanatengwa na kubaguliwa ndani ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Watu wasiojua historia ya taifa hili ndio wanaoeneza propaganda za kipuuzi kuwa Kigoma irudi Burundi, kwa bahati mbaya sana watu wa aina hiyo ndio walioajiriwa Serikalini "Uhamiaji" na wanaendeleza ubaguzi unaoweza kuligawa taifa.

Inashangaza sana, Rais wetu ana nasaba na waarabu lakini hakuna anaepaaza sauti kuhoji uhalali wake kuwa Rais, lakini muha wa Kigoma kuonekana kwenye eneo lake ndani ya Afrika ni kosa linalostahili kifo ? Hii dhambi ya kubaguana ndani ya JMT itakuja kupata majibu siku za usoni kama haya yanayotokea sasa kule Gaza, kati ya waisrael na wapalestina.
Hamna mtu anabagua Waha. Waha au wakazi wa Kigoma ni raia halali wa nchi kubwa na ya kujivunia ya Tanzania. Changamoto za mipakani zinawakabili pia wakazi wa Namanga, Ileje, Tunduma, Holili, Mtwara au Kagera.

Usikimbie Tanzania, hakuna nchi nzuri kama Tanzania
 
Nikimbizwe na nini nchi hii wakati uasisi wake nimeushudia tangu utoto? ... Umetaja Namanga Tunduma Ileje n.k, kama huko kote ni mipakani kwa nini Kigoma iwe na nongwa?... Inashangaza sana nchi kubwa kama Tanzania watendaji wake wanavyo zihofia Rwanda na Burundi.
 
Back
Top Bottom