Peter Msechu acha comedy kwenye afya yako, utakufa premature utuachie mkeo, watoto wako watateseka

mdukuzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
20,925
Reaction score
51,688
Hakuna ajuaye atakufa lini, ila kuna life style usipozingatia unajiwahishia mwenyewe kaburini,
Tupac nilijua atauliwa tu baafa ya diss track ya Hit them up, Amina Chifupa alijua atakufa baada ya kusema atawataja wauza udaga, Langa, Mangwea walijiwahisha mbele za haki sababu ya udaga, huenda wangekuwa hai mpaka leo, ulale na malaya bila kinga au uendeshe gari kwa speed kali 130 useme ajali kazini...hakika utakufa.

Captain John Komba alikuwa mwili nyumba, shati lake unaweza kufunikia gari aina ya IST, Lemutus Tshirt yake ungeweza kutengenezea tent, yule mwanamziki wa marekani ni Big Punisher alifia usingizini premature sababu ya tumbo kama lako, mwenzake Fat Joe machale yakamcheza akapunguza kilo kutoka 150 mpaka 80.

Nimekumbuka kitu kuhusu Capt Komba, siku zake za mwisho aliwahi kusema atakayemsaidia kupungua mwili wake atampa zawadi, alishaona hatari mbele yake, leo hayupo mkewe bado mbichi kabisaa.

Bwana mdogo Peter Msechu sio kwamba Mo Dewji hana hela ndio maana hanenepi, Bill Gates, Dangote, Kikwete wanaweza kufuga matumbo wakiamua ila wanajua madhara yake.

Kuwa serious na afya yako acha comedy na uhai, najua jitihada zako za kuwekewa puto ila zimekaa kikomedy comedy huenda hata sio kweli.

Wewe ni bingwa wa nyimbo za misiba, marafiki zako na ma DJ watapiga sana nyimbo zako siku ukifa wakati uwezo wa kukusaidia wanao sasa ila wanaona hauko serious.
Kila nafsi itaonja mauti ila kutangulia mapema sio powa
 
Watu wanene ninaowajua Walibarikiwa kuwa na Akili Kubwa ( Intelligent ) kwa Mimi najua alikuwa ni Hayati Mkapa tu pekee, ila kwa Wengine huwa ni 95% Fools. Hata Mwalimu wangu Mmoja wa Saikolojia aliwahi kuniambia huwezi kuwa Mnene sana ( kama alivyo Peter Msechu Pichani ) halafu ukawa na Akili Kubwa ( Mwerevu ) na ikitokea ukamkuta Mtu wa aina hiyo basi jua kapata tu bahati kutoka kwa Mungu.
 
Kama anaelewa madhara ya uzito uliopitiliza, sisi ni nani tuanze kumuundia tume.

Mtu na mwili wake, yeye ndiye anayejielewa vizuri sana kuliko sisi wapenzi watizamaji.

Tunachotakiwa kufanya, kila mtu kuyaishi maisha yake.

Ya Msechu tumuachie Msechu na ya Mdukuzi tumuachie Mdukuzi.​
 
Kuna ukweli kabisa
 
Huo mwili ndiyo Brand yenyewe, ndiyo duka, ndiyo kitega uchumi, unataka apungue ili afilisike na kufa njaa?
 
Wewe na huyo mwalimu wako na hata pita msechu wote hamna akili
 
Ule ni ugonjwa mkuu,sema ugonjwa upo kwa mjinga mmoja,ujinga,maradhi na umasikini ni mapacha watatu,alichelewa kuingia mjini bado ana mentality kuwa kitambi ni dill bado,
 
Umempa ushauri mzuri sana.

Zipo nyie nyingi na salama za kupunguza uzito japo ni za Gharama lakini Peter Msechu hawezi kushindwa
 
Sisi tunamshauri tu. Kuchukua hatua ni wajibu wake.
 
Watu na maishΓ  ya watu mkuu πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…

Msechu kuwa mnene Kuna mtu anateseka uko na kumwanzishia mada kbs πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜….

Unakuta asubuh msechu mwenyewe kashakula mkate mzima na mayai matano ,akisoma Uzi km huu anacheka Kwa dharau πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
Sie tutaedit nyimbo zake za misiba kwenye jpm,mkapa na mwinyi, tunaweka peter

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…