DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Msanii Peter Msechu ametoa kauli yake ya kukanusha kutoa wimbo unaosambaa Mitandaoni kwa sasa wa kuichafua Serikali akisema huyo sio yeye kabisa'
Kupitia Insta yake Msechu amweka video ya maelezo na kuandika ujumbe unaosema kwamba ....
TAARIFA KWA UMMA
Uongozi wa Msechu Entertainment Limited unapenda kuutarifu umma kuwa kumekua na maudhui ya sauti na picha zinayozunguka au kusambaa mtandaoni zinazodaiwa kuwa ni za Peter Joram Msechu, maudhui hayo ni bandia na hazijatolewa na uongozi wetu.
Tunasema kwa uwazi kwamba:
1. Maudhui hayo ni ya uongo na yametengenezwa kwa nia ya kupotosha umma.
2. Hakuna nyimbo, taarifa au maudhui mapya yaliyotolewa rasmi na Peter Joram Msechu katika kipindi hiki.
3. Kusambaza maudhui haya ni kitendo cha kihalifu, na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wanaohusika.
4. Tunawaomba Watanzania na mashabiki wote kupuuza na kutoendeleza usambazaji wa taarifa hizi.
5. Taarifa rasmi za Peter Joram Msechu zinapatikana kwenye kurasa zetu zilizoidhinishwa pekee.
Tunawashukuru kwa uelewa na kwa kuendelea kutuunga mkono.