Peter Msechu asema hajawahi kuona Watu ' Wanafiki ' na ' Wabinafsi ' duniani kama Watanzania

Peter Msechu asema hajawahi kuona Watu ' Wanafiki ' na ' Wabinafsi ' duniani kama Watanzania

Yeye ndo mnafiki wa kwanza kisha wanafuata watanzania alafu mimi ndo wa mwisho.

Si aliiimbia CCM mbele kwa mbele mwaka 2015 acha sasa imlalie mbele. Leo bungeni nimeshangaa naibu spika kuizima hoja ya kuzifungia nyimbo zao sasa wapate akili sio 2020 wawatungie nyimbo mawe na kiranja wao wa kuzimu
Akili yako imejaa siasa mdogo wangu relax maisha mafupi sana jadili kilichopo
 
Hivi Msechu na yule mdogo wake Mange Kimambi ,anaitwa Anil nani kibonge zaidi?
 
Akizungumza muda mfupi tu uliopita katika mahojiano na Kituo kimoja cha Television Msanii Peter Msechu amesema kwamba kama kuna kitu ambacho amejifunza kwa Watanzania basi ni tabia zao kubwa mbili ' pacha ' za Unafiki na Ubinafsi.

Alitolea mfano hai kwamba kuna siku moja aliwahi ' Kuposti ' Mtandaoni kuwaomba Watanzania wapakue Nyimbo zake na wampigie Kura lakini cha Kushangaza ndani ya Siku tatu alipata ' mrejesho ' wa Watu wasiozidi 25 tu lakini Kesho yake ' akaposti ' kuwa ameachana na Mkewe Mama Lolo cha kushangaza ndani ya dakika 10 alipokea sms zaidi ya 3200 za Watu huku wengine hata hawajui na wakijifanya kumpa ushauri na kumpoza na akashangaa mno kwamba iweje alipowataka wampe ' sapoti ' katika Kazi yake hawakumpa ' ushirikiano ' ila kwa mambo ya ' Kimbea ' ndipo wengi walijotokeza?

Nami nimuambie tu Peter Msechu kwamba nampa pole kubwa kwa kuchelewa Kwake kujua kwamba hakuna Watu ' Wanafiki ' na ' Wabinafsi ' duniani kama Watanzania na nadhani hicho ' Kipaji / Kipawa / Talanta ' pekee tuliyojaaliwa nayo Watanzania na kwakweli tunatendea haki kabisa.

Nawasilisha.

Ni bahati mbaya kachelewa kuwafahamu WaTz. Generally tunapenda cheap news kuliko hard news na utekelezaji wa mambo yetu upo hivyo.
Mfano, pitia kwa muuza magazeti yoyote asubuhi utashuhudia watu wapo busy na EPL kuliko mambo muhimu ya hapa Tz yanayohusu ustawi wa maisha yao
 
Y
Ni bahati mbaya kachelewa kuwafahamu WaTz. Generally tunapenda cheap news kuliko hard news na utekelezaji wa mambo yetu upo hivyo.
Mfano, pitia kwa muuza magazeti yoyote asubuhi utashuhudia watu wapo busy na EPL kuliko mambo muhimu ya hapa Tz yanayohusu ustawi wa maisha yao
Yeye si aliamua kuungana na watawala ambao ni wanyonyaji na kuamua kuwasifia? Sasa awaombe haohao watawala wampigie kura sisi watanzania tutabaki kufuatilia udaku...mambo ya kumuinua watamuinua anaowasifia kila siku...sisi vya kumuinua havituhusu
 
Hajakosea,leo hakuna mtu anahangaika na bajeti wala ripoti ya CAG,wanafuatilia chupi ya nandy na video za daimond
 
Pumbavu. Anatutukana kwa sababu alitaka tumpigie kura na hakupata alizotaka?
Yeye ndie mnafiki mkubwa. Amepata mshahara wake
 
Sisi ndio sisi, wachawi sisi, CCM sisi, wanga sisi, husuda sisi, uzandiki sisi, unafiki sisi, Kila kitu kibaya sisi. Hii ni laana ya mwenge.
Isaya 50;11

11 Tazama, ninyi nyote mwashao moto, mjifungiao hiyo mienge; endeni ninyi katika mwali wa moto wenu, na katikati ya mienge mliyoiwasha. Mtayapata haya kwa mkono wangu; mtalala kwa huzuni.
Isaya 50 :11
 
Hahaahahaaa...

Mchechuuu...

Pole kwa kuchelewa.
 
...Alitolea mfano hai kwamba kuna siku moja aliwahi ' Kuposti ' Mtandaoni kuwaomba Watanzania wapakue Nyimbo zake na wampigie Kura lakini cha Kushangaza ndani ya Siku tatu alipata ' mrejesho ' wa Watu wasiozidi 25 tu lakini Kesho yake ' akaposti ' kuwa ameachana na Mkewe Mama Lolo cha kushangaza ndani ya dakika 10 alipokea sms zaidi ya 3200 za Watu huku wengine hata hawajui na wakijifanya kumpa ushauri na kumpoza na akashangaa mno kwamba iweje alipowataka wampe ' sapoti ' katika Kazi yake hawakumpa ' ushirikiano ' ila kwa mambo ya ' Kimbea ' ndipo wengi walijotokeza?
Basi siku nyingine awe mjanja; aseme "Naombeni mpakue nyimbo zangu na mnipigie kura vinginevyo nitaachana na me wangu Mama Lolo"
Bila shaka watu watapakua nyimbo na kumpigia kura sambamba na kumpa ushauri asimuache Mama Lolo
 
Back
Top Bottom