Peter Msigwa atoke kabla hajawa Kirusi ndani ya CHADEMA

Mpwayungu Village

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
14,540
Reaction score
30,875
Huu mwaka ni mbovu kwa wananchi tangu dunia iumbwe, chama cha CHADEMA kinapitia wakati mgumu sana, viongozi wakuu, viongozi wa Kanda na mikoa wamepigwa gundi mdomoni kuongea hawawezi tena na huenda Kuna void contract iliyowekwa baina ya hawa viongozi wa CHADEMA tunaodhani ni watetezi na hawa Chama cha Mapinduzi.

Naomba twende Sawa :iko hivi hiki Chama tawala kinatumia mbinu nyepesi sana kuongoza hii nchi. Hii mbinu ya kugawa pesa ovyo ni rahisi kwao kwasababu hizi pesa hawatafuti wao Bali ni sisi watanzania. Sasa huyu mama anatumia fund nyingi kuwapa viongozi wakuu wa upinzani na ndio maana huoni Mbowe kaongea suala la Ngorongoro wala Katibu Mkuu mzee wa kutweet kila tukio lakini Hola. Muda utasema ila kwa hili la Peter Msigwa kuwekwa kwenye kamati ya uwekaji mipaka Loliondo ni ishara ya wazi ya usaliti ndani ya chama na kwa Watanzania.

Ni ajabu sana, unamuweka Peter Msigwa na Steve Nyerere kwenye uwekaji mipaka Loliondo na Ngorongoro wanajua kitu gani hawa juu ya land measurements and surveying.

Hili suala ni la kitaaluma na linahitaji wenyeji wa maeneo hayo sasa Serikali inaliendesha kisiasa.

Binafsi kwa mtazamo wangu tumwache Peter Msigwa aende anakotaka, kuendelea kuwa CHADEMA ni nembo tu ila picha halisi haipo hapo.

Huyu mtu ni kaidi sana na anajionaga mtu wa demokrasia na hakuna wa kumfanyia judgements, anaona anategemewa ndani ya chama, ni msomi, ana nguvu kumbe useless kabisa.

"when injustice becomes law, resistance becomes duty" ~Americas former president said.
 
CHADEMA wamekua wajinga, sasa hivi chama kinaendeshwa na martin maranja, mdude na hilda newton hawa ni vilaza waliovamia siasa! nashaanga eti mtu kama martin anamtukana msigwa yaani kuripoti kesi ya mbowe kutoka mahakamani na kuchangiwa zile buku buku na watu ameshajiona ni mkubwa pale Chamani ilihali hafiki hata asilimia moja ya msigwa,

Chama kinauwawa kwa ujinga wa wanaojiita wanaharakati wa Twiter

Watu wa maana wametulia mmebaki na Hilda Newton, mdude na masese akili hamna
 
Msigwa amekosa maarifa, ameshindwa kuzicheza karata zake vizuri, huwezi kuitwa mwanasiasa mkomavu bila kuwa na ngozi ngumu.
 
hao njaa zao tu hakuna mkono wa mama kwenye hil
 
Msigwa amekosa maarifa, ameshindwa kuzicheza karata zake vizuri, huwezi kuitwa mwanasiasa mkomavu bila kuwa na ngozi ngumu.
Ngozi ngumu kwa nani? Karata mchezee nani? Watanzania wengi wameshachoka na hata hawafahamu kwanini wanaishi na wenzetu huko Duniani wanaishaje, hataupige kelele vipi hawatakuelewa sababu wote njaa zimehamia vichwani. Naamini hata wewe ungepata hii asali usingeicha.
 
Siasa ni kukubaliana kutokubaliana na siyo kufukuzana!! Ukinzani ndo ukubwa!

Mbona Polepole, Gwajima, akina Ole Sendeka, Mpina kila siku wanaenda kinyume na serikali ya CCM na hawafukuzwi!!

Waache wakue pamoja ndo ukubwa huo!!
 
Msigwa naye hajielewi, utetezi wake kwa mambo ambayo serikali inafanya unaisaidia zaidi Kampuni ya Mwarabu wa OBC na kuwakandamiza wamasai.

Hivi Msigwa anataka kujitoa ufahamu kuwa kampuni hiyo ya Mwarabu ya OBC imekuwa ikilitaka eneo hilo la wamasai la Loliondo kwa miaka mingi tu?
 
Huu mwaka ni mbovu kwa wananchi tangu dunia iumbwe, chama cha CHADEMA kinapitia wakati mgumu sana, viongozi wakuu, viongozi wa Kanda na mikoa wamepigwa gundi mdomoni kuongea hawawezi tena na huenda Kuna void contract iliyowekwa baina ya hawa viongozi wa CHADEMA tunaodhani ni watetezi na hawa Chama cha Mapinduzi.

Naomba twende Sawa :iko hivi hiki Chama tawala kinatumia mbinu nyepesi sana kuongoza hii nchi. Hii mbinu ya kugawa pesa ovyo ni rahisi kwao kwasababu hizi pesa hawatafuti wao Bali ni sisi watanzania. Sasa huyu mama anatumia fund nyingi kuwapa viongozi wakuu wa upinzani na ndio maana huoni Mbowe kaongea suala la Ngorongoro wala Katibu Mkuu mzee wa kutweet kila tukio lakini Hola. Muda utasema ila kwa hili la Peter Msigwa kuwekwa kwenye kamati ya uwekaji mipaka Loliondo ni ishara ya wazi ya usaliti ndani ya chama na kwa Watanzania.

Ni ajabu sana, unamuweka Peter Msigwa na Steve Nyerere kwenye uwekaji mipaka Loliondo na Ngorongoro wanajua kitu gani hawa juu ya land measurements and surveying.

Hili suala ni la kitaaluma na linahitaji wenyeji wa maeneo hayo sasa Serikali inaliendesha kisiasa.

Binafsi kwa mtazamo wangu tumwache Peter Msigwa aende anakotaka, kuendelea kuwa CHADEMA ni nembo tu ila picha halisi haipo hapo.

Huyu mtu ni kaidi sana na anajionaga mtu wa demokrasia na hakuna wa kumfanyia judgements, anaona anategemewa ndani ya chama, ni msomi, ana nguvu kumbe useless kabisa.

"when injustice becomes law, resistance becomes duty" ~Americas former president said.
Hoja tofauti ni nzuri kwa AFYA ya democracy.

Kama amekubali kuingia ktk kamati hiyo ilojaa manunguniko ya wananchi ni DOA kwake na amevuka mipaka.

Tatizo pia ni viongozi kutoweka bayana msimamo wa Chama kuhusu jambo Hilo.

Wasiwe wanakaa kimya.
 
CHADEMA wamekua wajinga, sasa hivi chama kinaendeshwa na martin maranja, mdude na hilda newton hawa ni vilaza waliovamia siasa! nashaanga eti mtu kama martin anamtukana msigwa yaani kuripoti kesi ya mbowe kutoka mahakamani na kuchangiwa zile buku buku na watu ameshajiona ni mkubwa pale Chamani ilihali hafiki hata asilimia moja ya msigwa,

Chama kinauwawa kwa ujinga wa wanaojiita wanaharakati wa Twiter

Watu wa maana wametulia mmebaki na Hilda Newton, mdude na masese akili hamna
Umesahau kwamba kigogo aliwahi kuwa zaidi ya kamati kuu ya chama
 
Back
Top Bottom