Peter Msigwa ni mlaji wa matapishi yake

Peter Msigwa ni mlaji wa matapishi yake

Tulitegemea kauli za kipumbavu kama hizi zako toka kwa nyumbu wa CHADEMA. Nyie mtu kuhama chama ni kosa la jinai na sio haki ya kikatiba. Hiyo katiba mpya mnayotaka haitatoa uhuru wa mtu kuhama CHADEMA? Wewe Nanyaro ni CHADEMA mchana ila usiku ni CCM. Bora Mdude ambaye kajitoa ufahamu kuliko nyie mandumilakuwili ambao mko kotekote.
Wewe ni kiazi! Una utapiamlo ambao umeadhiri uwezo wako wa kufikiri
 
Njaa ilimtoa ccm akafata shibe chadema njaa imetoa cdm.
Angehama kipindi kile ndugu yake angawa pesa za kununua wapinzani
 
Peter Msigwa Mlaji wa matapishi yake

Uamuzi wa Peter Msigwa kuhama kutoka Chadema kwenda CCM unaacha alama mbaya katika siasa za Tanzania. Ni tukio linalofungua mjadala kuhusu uaminifu, uadilifu, na misingi ya uongozi. Msigwa, aliyewahi kuwa kiongozi mashuhuri ndani ya Chadema, sasa anaonekana kama kiongozi aliyeshindwa kuhimili changamoto na kushikilia misingi ya chama chake. Hii ni fundisho kwa viongozi wengine kwamba uaminifu na uadilifu ni muhimu zaidi kuliko madaraka, na kwamba kiongozi bora ni yule anayesimama imara katika misingi na itikadi zake, bila kujali ugumu wa hali. Wanachama na wafuasi wa Chadema wanapaswa kuendelea kushikilia misingi ya chama na kuwapinga wale wanaosaliti kwa maslahi binafsi


1. Kula Matapishi Yake Mwenyewe

Peter Msigwa alishawahi kusema hadharani kwamba, endapo angehama Chadema, basi nyumba na mali zake zichomwe moto. Kauli hii ilionesha kiwango cha kujitolea na uaminifu wake kwa Chadema. Leo hii, kwa kuhama kutoka Chadema na kujiunga na CCM, Msigwa amekula matapishi yake mwenyewe. Hii ni ukosefu wa msimamo na uaminifu kwa maneno yake mwenyewe. Kula matapishi ni jambo linaloonekana kwa waoga tu; wale ambao hawawezi kusimama imara katika misingi na maamuzi yao, hasa wakati wa changamoto

2. Akili Ndogo na Kukosa Uvumilivu

Msigwa amedhibitisha kuwa yeye ni akili ndogo. Akili kubwa huwa na uwezo wa kuhimili changamoto zote nyakati zote, bila kujali ugumu wa hali. Katika maisha ya kisiasa, changamoto ni sehemu ya kawaida, na kiongozi mwenye akili kubwa anajua jinsi ya kuvuka vipingamizi bila kuhatarisha uaminifu na itikadi zake. Kuhama kwake Chadema kwa sababu ya kukosa nafasi ya uongozi inaonesha wazi kuwa alikosa uvumilivu na ujasiri wa kukabiliana na changamoto hizo

3. Usaliti kwa Watu wa Iringa

Kuhama kwa Msigwa ni usaliti mkubwa kwa watu wa Iringa waliomchagua na kumwamini kama kiongozi wao. Usaliti ni kitu kibaya mno kwa binadamu, kwani unavunja imani na uaminifu ambao umejengwa kwa muda mrefu. Wananchi wa Iringa walimtegemea Msigwa kwa kuwa alikuwa sauti yao, mtetezi wa haki na maendeleo yao. Kuhama kwake kunawaacha wananchi hawa wakiwa na hisia za kukatishwa tamaa na kuhisi kusalitiwa,

4. Kukosa Uadilifu na Uaminifu

Msigwa amekosa uadilifu na ni wazi hata huko CCM hatoaminika. Alikuwa ndani ya Chadema kwa kuwa alikuwa kiongozi, lakini ameshindwa kuendelea kuwa mwanachama wa kawaida baada ya kupoteza nafasi za uongozi. Hii inaonesha kuwa uaminifu wake kwa Chadema ulikuwa wa juu juu na ulitokana na maslahi binafsi ya madaraka. Uchu wa madaraka, ulafi na ulevi wa madaraka ni tabia zinazoonesha kiongozi asiye na msimamo na asiyeaminika. Wananchi na wafuasi wa Chadema walimwamini Msigwa kama kiongozi mwadilifu, lakini hatua yake ya kuhama inaonesha kuwa alikuwa na ajenda za kibinafsi zaidi kuliko maslahi ya watu

5. Kukosa Busara na Hekima

Msigwa amekosa busara na hekima. Angeweza kukaa kimya baada ya kuondoka Chadema, lakini kuanza kuukejeli Chadema ni kiwango cha juu cha upumbavu na upofu. Kiongozi mwenye busara na hekima anajua kwamba ni bora kuondoka kwa heshima bila kushambulia chama ambacho kilimlea na kumkuza kisiasa. Kejeli na maneno ya kukashifu yanayotolewa na Msigwa baada ya kuhama Chadema yanaonesha ukosefu wa heshima na unyenyekevu. Hii ni tabia inayovunja moyo na kuonesha kwamba hajafikiria kwa kina kuhusu athari za maneno na matendo yake kwa wafuasi na wanachama wa Chadema

Nanyaro EJ
Sioni ajabu...
Kama chadema chama kizima kilikula matapishi kwa kumchukua Hayati Lowassa ambaye walizunguka nchi nzima wakisema ni fisadi, na mkawaangua mkono, basi sioni jabu kwa msigwa.
Mwanasiasa ni wmanasiasa tu hapiganii maslahi yako bali tumbo lake. Kwanza kuwapigania watu kama watanzania ni kazi kuliko kazi yenyewe
 
nadhani hata wale aliowaacha chadema pia wana tabia zinazoendana rejea makaribisho ya hayati lowassa.
 
Back
Top Bottom