Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Hata hivyo, Dk Mwakyembe alisema, Dk Msabaha akiwa nje ya kiapo alieleza kamati kwamba, yeye ni mbuzi wa kafara kwa sababu biashara hiyo ilikuwa ya Lowassa na mshirika wake, Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz.
Rostam aliandamwa sana alipodai kuwa kampuni zake zimetoa ajiri kwa watu zaidi ya 6,000. Sasa humu tunaambiwa kuwa kampuni yake ya Mirambo ina asilimia 35 za share za Vodacom. Hivi Vodacom imetoa ajira kwa watu wangapi Tanzania? Kuanzia hao wa maofisini kwake, wauza vocha n.k.? Hawajafika 6000? Bado Caspian ambaye yumo sana kwenye migodi! Kwa kutanguliza chuki na munkari kwenye suala hili, hatutafika kokote. Kama kweli mnataka kumuwajibisha Rostam itabidi mtulie na kupanga mikakati iliyo bora kuliko hii iliyojazana humu!
Amandla........
Rostam aliandamwa sana alipodai kuwa kampuni zake zimetoa ajiri kwa watu zaidi ya 6,000.
Sasa humu tunaambiwa kuwa kampuni yake ya Mirambo ina asilimia 35 za share za Vodacom.
Hivi Vodacom imetoa ajira kwa watu wangapi Tanzania? Kuanzia hao wa maofisini kwake, wauza vocha n.k.? Hawajafika 6000?
Bado Caspian ambaye yumo sana kwenye migodi! Kwa kutanguliza chuki na munkari kwenye suala hili, hatutafika kokote.
Kama kweli mnataka kumuwajibisha Rostam itabidi mtulie na kupanga mikakati iliyo bora kuliko hii iliyojazana humu!
Amandla........
Kwa nini Msabaha aliyasema haya nje ya kiapo? Unadhani atakuwa na ubavu wa kuyarudia hadharani? Au Mahakamani ambako nako kuna kiapo? Huyu kweli ni mtu wa kumuamini?
Amandla........
4. Lowassa amehusishwa na upendeleo wa kampuni hiyo kutokana na barua yake Juni 21, 2006 akiagiza kuwa Richmond ipewe zabuni
5. Alisema kamati haikufurahishwa na taarifa zinazomgusa moja kwa moja Lowassa katika kupendelea Kampuni ya Richmond Development
6. Hata hivyo, Dk Mwakyembe alisema, Dk Msabaha akiwa nje ya kiapo alieleza kamati kwamba, yeye ni mbuzi wa kafara kwa sababu biashara hiyo ilikuwa ya Lowassa na mshirika wake, Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz.
- Mkuu mimi ndiye hasa nimemuandama Rostam kwa kauli yake kwamba ameajiri wafanyakazi 6000, huku akiwa hana kampuni hata moja iliyoandikishwa kwa jina lake, kama Mengi. Kama hoja yako ni valid basi angesema kampuni zinazomilikiwa na familia yangu, tumekuomba sana uzitaje umeshindwa kabisaa sasa unajaribu kuhalalisha hoja yake Rostam kwa habari ambazo hazina uhakika, ninakuomba tena hebu zitaje kampuni zzinazomilikwa na familia yake kwa sababu Brela hakuna kampuni hata moja iliyosajiliwa kwa jina lake, au familia yake!
- Kampuni ya Caspian haiko kwa jina lake, na wala yeye sio majority share holder, meaning kwamba anaficha something, sasa ni nini hasa anachoficha?
Sasa hivi kazi ni moja tu nayo ni kukata mzizi wake wa urafiki na rais, then kumfikisha kwenye sheria, pole pole tunamkaribia maana kesi ya Mengi tayari iko mahakamani.
Respect.
FMES!
Hii ni kutoka hoja kuu ya mzee Mwanakijiji.Mfanyakazi wa BOT ambaye ana uwezo na fedha ya kuanzisha kampuni ya Planetel (ningependa kweli kujua kampuni hii ilianzishwa lini na wana hisa wake!) na kuwa na hisa kubwa tu kule Vodacom ambazo walikuwa waziuze (sijui kama tayari wameziuza) kwa kampuni ya Mirambo inayomilikiwa na Rostam!
Rostam aliandamwa sana alipodai kuwa kampuni zake zimetoa ajiri kwa watu zaidi ya 6,000. Sasa humu tunaambiwa kuwa kampuni yake ya Mirambo ina asilimia 35 za share za Vodacom. Hivi Vodacom imetoa ajira kwa watu wangapi Tanzania? Kuanzia hao wa maofisini kwake, wauza vocha n.k.? Hawajafika 6000? Bado Caspian ambaye yumo sana kwenye migodi! Kwa kutanguliza chuki na munkari kwenye suala hili, hatutafika kokote. Kama kweli mnataka kumuwajibisha Rostam itabidi mtulie na kupanga mikakati iliyo bora kuliko hii iliyojazana humu!
Amandla........
Hii ni kutoka hoja kuu ya mzee Mwanakijiji.
Mimi huniamini basi hata mzee mwanakijiji humuamini? Umeingiaje kwenye mjadala bila kusoma hoja kuu? Au unataka kutuambia kuwa Mzee Mwanakijiji anamsingizia Rostam maana yeye si mmiliki wa Caspian au Mirambo? Tuelewe lipi! Kwa vile unajua kuwa Mzee Mwanakijiji kamsingizia Rostam, basi tueleze ni nani mwenye hizo kampuni. Si ulishacheki mpaka Brela! Na unawajua ndugu wote wa Rostam kiasi cha kusema hakuna ndugu yake kwenye hizo kampuni! Chonde chonde, Mkuu.
Amandla.......
Hii ni kutoka hoja kuu ya mzee Mwanakijiji.
Mimi huniamini basi hata mzee mwanakijiji humuamini? Umeingiaje kwenye mjadala bila kusoma hoja kuu? Au unataka kutuambia kuwa Mzee Mwanakijiji anamsingizia Rostam maana yeye si mmiliki wa Caspian au Mirambo? Tuelewe lipi! Kwa vile unajua kuwa Mzee Mwanakijiji kamsingizia Rostam, basi tueleze ni nani mwenye hizo kampuni. Si ulishacheki mpaka Brela! Na unawajua ndugu wote wa Rostam kiasi cha kusema hakuna ndugu yake kwenye hizo kampuni! Chonde chonde, Mkuu.
Amandla.......
For some resorn kuna watu wengi tu wanamakampuni Under trust. Ukiwa na kampuni sio lazima jina lako liwe kwenye shareholders list. Kuna watu wengine wanawatumia their attoney to represent their shares therefore I dont see any problem
- Mkuu jibu hoja zangu, kama huwezi kubali tu usijaribu kutuchanganya maana tunazo akili za kutosha kujua kwamba Rostam ni fisadi kama alivyosema Mzee Mengi, ulianza vizuri sasa vipi tena?
- Jibu hoja mkuu, mimi sio Mwanakijiji yeye anazo hoja zake sasa usituchanganye hapa, kama huwezi jibu ni kukubali tu mkuu!
FMEs!
Hoja gani tena, Mkuu? Mnajicontradict wenyewe halafu unanilaumu mimi! Mzee Mwanakijiji ndiye aliyeleta hoja mama hapa sasa wewe unataka tumdharau tukusikilize wewe? Mzee Mwanakiji ambae si mshabiki wa Rostam by all means anasema hizi kampuni ni za Rostam na wewe ambae nawe si shabiki wa Rostam unasema si zake, sasa tumuamini nani? Mbona unashindwa kutueleza hizo kampuni za Caspian na Mirambo ni nani wameorodheshwa kama wamiliki? Ni lazima uwajue maana unajua kuwa si Rostam wala ndugu zake wameorodheshwa! Hili nalo lina ugumu gani? Au hauwajui il hali ulikuwa unafurahisha baraza! Na kama unavyodai, Rostam hamiliki kampuni yeyote (ikiwemo Kagoda) hayo mapesa ya EPA aliyachota vipi? Alikuwa anaenda dirishani BOT kupokea?
Tuoneeni huruma wenzenu. Hatuja soma lakini si punguwani kiasi hicho!
Amandla.........
Caspian Construction LTD ilipoanzishwa mwaka 1993 ilikuwa chini ya jina la nani?
- Ninasema hivi Brela hakuna kampuni hata moja iliyoandikishwa kwa jina la Rostam, lakini Rostma ameandikishwa kuwaajiri wafanyakazi wawili kwa jina lake nao ni dereva wake na secretary wake tu, sasa naomba kukuliza tena hao wafanyakazi 6000 amewaajiri kwenye kampuni gani?
- Fundi kubali kwamba huna hoja ila unataka kustarehesha baraza tu, kwa sababu Mwanakijiji sio hoja ya Rostam uliyoisimamia toka jana hapa, either unayajua majina ya kampuni za Rostam au huzijui kubali tu!
- Kusema neno sio punguwa ni rahisi sana tatizo ni kuthibitisha hilo neno ulilolieta mwenyewe, labda kwa kuonewa huruma ni wananchi wa Tanzania wanaolala giza huku Rostam akikusanya hela za umeme ambao hana hata kampuni ya kuuzalisha! Lakini anachukua hela mpaka leo!
Respect.
FMEs!
- Ilikuwa under Rostam lakini sio leo, haiko under hilo jina tena, vipi mkuu unajua sababu?
FMES!
Huko Brela wanaorodheshwa madereva na masekretari? Tena na mtu ambae hajaorodheshwa kama mmoja wa wamiliki wa kampuni husika! Mbona hautuonei huruma, Mkuu?
Amandla........
Sasa hivi iko kwa jina la nani basi? mbona unazunguka mbuyu?
Amandla............