RUTAJUMBUKIRWA
Senior Member
- May 3, 2009
- 185
- 89
Mch. Christopher Mtikila alimshambulia Peter Serukamba eti ni Mtutsi. Akasupport hoja yake kwa kusema eti ni Serugamba. Kwa mawazo ya Mtikila jina Serugamba linamfanya kuwa Mtutsi. Tumsamehe bule Mzee Mtikila, yeye ni M-Ludewa hajui chochote kuhusu mikoa ya magharibi mwa Tanzania. Kwanza niseme Watutsi si kabila lenye majina yake, wanachangia majina na watu wote wa Maziwa Makuu. Na waha, wahangaza, washubi, Warwanda, warundi wanaongea lugha moja na wana majina yanayofanana. Mfano utashangaa kukuta Zito Kabwe anaongea kilugha na Kagame, au Serugamba (sic Serukamba) ana-bonga lugha moja na rais wa Burundi Nkurunziza. Utashangaa Muha Bizman! mwana mziki, jina lake ni Bizimana, jina maarufu Burundi, ila yeye ni Muha. Mtoto wa Ntagazwa anaitwa Uwimana, jina maalufu Rwanda na Burundi, ila yeye ni Mha. Alafu pia Muha anaweza kuwa Mtutsi na bado akawa Mha. Mhangaza anaweza kuwa Mtutsi bado ni Mha. hawa jamaa wametawaliwa na machifu wa Ki-Tutsi karne wa karne, akina Nzogera, Ntare, etc. Lakini mjadala unavyokwenda kila mwenye sura ya Kitutsi anaitwa eti si Mtanzania. wanamnyanyasa sanaana, magazeti yanayoandikwa na watu wasioelewa wanaanza kuwafanyia propaganda chafu. Mfano ni Mzee Nyambere Mushengezi. alivyokuwa TRA kama head of Corporate Affairs, magazeti yalipiga majungu, watu wakapiga midomo eti Mnyamlenge yupo TRA! Sasa mbona watu wameumbuka? Mbunge wa Ngara Ntukamazina. watu walipiga majungu, wakayawaya, eti Mtutsi yupo Ikulu. wakati huo alikuwa ni katibu utumishi. Aibuu ya ubaguzi. Jeshini alikuwepo Luteni Kanali mmoja Mha anaitwa Ruzoka, maskini bungeni ikafika eti jeshini kuna Banyamulenge, etc. Baadae akafukuzwa, muha wa watu, kosa lake kuonekana na sura ya Kitutsi. Mbona wenye sura ya Kihutu hawaguswi? Ubaguzi mbaya, achene, Tanzania ni moja Dar-Ngara, Mtwara hadi Karagwe, Ruvuma hadi Sirare.