Burial ni wimbo ambao uko kwenye albamu ya Legalize It. Nyimbo kama Here Comes The Judge, Maga Dog alizifyatua mwishoni wa miaka 1960 na mwanzoni wa miaka 1970 kabla hajajitoa THE WAILERS pamoja na Neville O'Rilley Livingstone a.k.a Bunny Wailer/Jah B/The Blackheart Man. Sababu iliyopelekea Wailers kusambaratika moja wapo ni Chris Blackwell mmiliki wa Island Records alikuwa anamsukuma Marley kama the main guy at the expense ya Tosh na Wailer. sababu nyingine ni kwamba nyimbo nyingi zilizokuwa zinaappear kwenye album za Catch a Fire and Burning zilikuwa zinatambulishwa kama mtunzi ni Marley pekee bila kushirikisha mchango wa Tosh na Wailer, vile vile Marley alikuwa anachukua lead vocals kwenye nyimbo nyingi za album tajwa tofauti na wenzake, nyimbo chache kama stop the train, 400 years and you can't blame the youth, Tosh alikuwa lead vocals na Bunny alikuwa lead vocal kwenye Haleluyah Time. Baada ya Tour ya UK, Bunny Wailer alikataa kutour USA ambapo nafasi yake ilizibwa na Marehemu Joseph (Joe) Higgs, sababu iliyotolewa wakati huo inasemakana alikuwa anaogopa kupanda ndege, ila kuna interview aliulizwa alidai alikataa kutour sababu aliona Blackwell/ Whitewell/ Whiteworst anawapeleka siko ana alifikiri Bob na Peter watamuunga kwa msimamo huo ila wenzake hawakufanya hivyo. Tosh alikuwa anataka kutoa single zake kupitia Island lakini Whiteworst alimgomea na ukizangitia uhusiano wake na Marley pamoja Whiteworst ulizorota mno akaamua kujiondoa. Walikuja kuperform pamoja kwenye concert 1974 na Marvin Gaye na ya mwisho kuperform pamoja ilikuwa kwenye concert ya wonder dream concert for the benefit of blind ambapo headliner alikuwa Steve Wonder.