Petisheni dhidi ya Diamond Platnamz ili kumzuia kushiriki BET Awards haina mashiko

Petisheni dhidi ya Diamond Platnamz ili kumzuia kushiriki BET Awards haina mashiko

Watanzania sisi ni watu wa kipekee sana duniani. Hebu tujiulize masuala yafuatayo.

1. Mange kimambi aliitisha Maandamano April 26, 2020, mtanzania yupi aliyejitokeza?

2. Chadema waliitisha Maandamano ya UKUTA, nani aliyesupport?

3. Kubwa zaidi Nov 1 waliitisha Maandamano ya amani kupinga Uchaguzi nani aliyeshiriki? Lissu alizuiwa Kibaha, siku nzima, alizuiwa kampeni siku 8, ni mtanzania yupi aliyeingia barabarani kuonyesha upingwaji wa jambo hilo?

Leo tunataka Diamond ndiye asimame kupigania haki zetu? Akikamatwa akafungwa nani atailisha familia yake? Leo mdudr nyangali yuko ndani, hata hela ya wakili inabidi itembeze bakuli? Tuache hayo, kuna wanamuziki kama Vitael Maembe wapigania haki wakubwa kimuziki, je wangapi tunasupport kazi zake?

Tunachukulia mfano wa wanaijeria. Well ni mfano mzuri lakini ni irrelevant. Nigeria kule music industry imekuwa na kwa kiasi kikubwa iko independent from the government, kwetu huku msanii gani anaweza fanya mziki bila kuwa na woga wa serikali kumbinya? Pili, wanaijeria wanaingia front kisha wasanii wanatoa support, huku sisi watanzania wanajifungia vyumbani wakiogopa kuumia, kufa au kupoteza kazi zao huku wakitaka wengine ndio wapiganie haki zao, Je wenyewe hawana familia? Tumuache Diamond atafute hela ya kupambana na umasikini. Kila mtu ashinde mechi zake.
 
Back
Top Bottom