Petit Man atangaza ndoa na dada wa Diamond

Petit Man atangaza ndoa na dada wa Diamond

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
MAPENZI bwana ! Baada ya kuogelea kwa muda mrefu katika penzi la muigizaji Kajala Masanja, hatimaye shemeji wa aliyekuwa rafiki wa mwigizaji huyo, Wema Sepetu, Ahmed Hashimu ‘ Petit Man ’ ametangaza ndoa na dada wa Mbongo Fleva , Nasibu Abdul ' diamond

Kwa mujibu wa chanzo chetu makini kilicho karibu na Diamond na Wema ambao penzi lao lilipata ‘ mushkeli ’ kidogo hivi karibuni, Petit Man tayari ameshakamilisha kila kitu kinachotakiwa kufanyika kabla ya ndoa na kilichobaki ni kutamka siku husika tu.

Kilidai kuwa, Petit alichukua uamuzi huo baada ya kushauriwa na Wema kuwa umri unakwenda na vishawishi ni vingi hivyo ni bora aoe mapema. “Unajua Petit Man anamheshimu sana Wema kwa hiyo alipomwambia Petit kuwa umri unazidi kwenda na anahitaji kuwa na familia yake akaukubali ushauri wake, ” kilinyetisha chanzo hicho.

Esma akipozi Baada ya kupata maelezo hayo, Ijumaa lilimtafuta Petit Man na kumuuliza kuhusiana na ishu hiyo, bila kuumauma maneno alikiri. “Ni kweli mama ( Wema ) aliniweka chini na kuniambia kuwa umri unakwenda hivyo nahitaji niwe na familia yangu kwa hiyo siwezi kuwa na familia bila ya kuwa na mke ndipo aliponichagulia mke ambaye ni dada yake wa damu kabisa na Nasibu Abdul Diamond anayeitwa Esma na kwa taarifa yako tu, tayari nimeshakamilisha kila kitu ,” alisema Petit .

Wakati akiwa na Kajala. Alipoulizwa kuhusiana na wanawake aliowahi kuwa nao kipindi cha nyuma akiwemo Kajala , Petit alisema huko kote ilikuwa ni njia ya kuelekea kwenye kilele cha mafanikio ambayo ni ndoa yake na Esma.

“Acha nipumzike na madhira ya dunia maana huko kote nilipopita hakukuwa chaguo langu ila kwa Esma nimekufa nimeoza bado kuzikwa tu yaani mimi ni mfu ninayetembea mbele ya Esma.

Chanzo: 2Jiachie

 
Huyu Petit naee mbona majanga wazo la kuoa kapewa na mama na mke kachaguliwa.
Mbona mama ake nae ajaolewa au umri wake umeganda.
 
huyo wema naye kumbe anaweza kushauri.. ivi umri wake bado miaka 22 ndo kaona wa petit umeenda.. Au kujishaua ndo domo amuone wa maana
 
Huyu Petit naee mbona majanga wazo la kuoa kapewa na mama na mke kachaguliwa.
Mbona mama ake nae ajaolewa au umri wake umeganda.

Ebu tupe uhondo kwanza, ila huyu mtoto anatafuta makuu, huyo shuga mami atamrisha nini au ndo atategemea vya shemeji, ila peti mjanja wewe hutak stress maana hamisa pasua kichwa yule angekuua shenzi type
 
Si niliskiaga huyu dogo alikua anakulana na martin kadinda...
 
Kwani Petit Man anafanya kazi gani inayomruhusu kuoa na kuwa na familia huyu jamaa si ni mdananda tu kweli ukistaajabu ya Musa..................
 
Kwangu mimi mtoto wa kiume akiongozana na mwanamke/wanawake wasio kuwa ndugu zake,wafanyakazi wenzie wala wapenzi wake 24/7 namuona -------.
 
Duh shetani anapokushauri uende kuabudu ujue ana sehemu anapanga kukupoteza,Wema ndo kamwambia umri unaenda aoe kweli kazi ipo.
 
Wema amewachokaa wanakula kila siku kwake ameona amshaurii ili wajiendee makwao maana washaona kwa wema ndio nyumbani kwaoo
 
hivi wema umri wake uko paused mbona nae haolewi...

Dah wa kuoa si ndo mpaka hapatikane we hadi domo kuandika ig atakuwa amemchoka ukichangia na life style lake hata arakaye mpata mume waendane naye kitabia bila hivo ni ngumu ukichangia na maskendo
 
Dah wa kuoa si ndo mpaka hapatikane we hadi domo kuandika ig atakuwa amemchoka ukichangia na life style lake hata arakaye mpata mume waendane naye kitabia bila hivo ni ngumu ukichangia na maskendo
amuoe tu hivo hivo kwani alimkuta msikitini kwamba aseme wema kabadilika?
 
Ameshauriwa kuoa na kuchaguliwa mke. Mbona yupo kama msukule wa Wema?
 
Back
Top Bottom