GE2025 Petro Ntagira (mwanafunzi MUST) achukua fomu kugombea Udiwani Iyunga, Mbeya

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Petro Daniel Ntagira, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST), ametangaza rasmi nia ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Udiwani katika Kata ya Iyunga, Jijini Mbeya.

Ntagira amesema amechukua hatua hiyo baada ya kupata msukumo wa kutumia taaluma yake ya Uhandisi kuisaidia jamii aliyoishi nayo kwa takribani miaka minne. Ametaja changamoto zinazowakabili wananchi wa Iyunga kuwa ni pamoja na ukosefu wa maendeleo kwa vijana na watu wasiojiweza, akisisitiza kuwa ana dhamira ya dhati ya kuzitatua kupitia uongozi wake.

"Ninaifahamu vizuri jiografia ya Iyunga na matatizo ya msingi ya wananchi wake. Nina ndoto ya kushirikiana nao kuleta mabadiliko chanya yatakayogusa maisha ya kila mmoja," amesema Ntagira.

Aidha, amewaomba wananchi wa Iyunga na Watanzania kwa ujumla kumuunga mkono kama kijana mwenye maono mapana ya kuifikisha Tanzania katika hatua mpya ya maendeleo, hususan kwenye nyanja ya kiuchumi.

Screenshot 2025-06-28 092114.png
 
Wapi papaa Joshua Mbilinyi mutu ya vitendeakazi tiba?
 
Kawaida tu hamna kipya,ukishindwa ulete mrejesho kama ulivyoleta habari yako
 
Back
Top Bottom