Mgogoro wa kisiasa katika Mashariki ya Kati, ambako Tanzania hununua sehemu kubwa ya bidhaa zake za mafuta, uliibuka upya katika mwezi Septemba 2026 na hivyo kuendelea kuathiri uzalishaji, upatikanaji na usafirishaji wa mafuta duniani.
Mgogoro huo umesababisha ongezeko kubwa la bei za mafuta yaliyosafishwa katika soko la dunia kwa mwezi Septemba 2026.
Kutokana na hali hiyo, kwa mwezi Oktoba 2026, bei za petroli, dizeli na mafuta ya taa nchini zimeongezeka ikilinganishwa na bei za mwezi Septemba 2026.
Serikali inaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa soko la mafuta duniani na kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa za mafuta nchini unakuwa endelevu na bei ni himilivu.
EWURA inatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini zitakazotumika kuanzia Jumatano ya tarehe 07 Oktoba 2026 saa 6:01 usiku. Kwa mwezi Oktoba 2026, bei za rejareja na jumla katika Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara ni kama zinavyoonekana katika Jedwali Na. 1 na 2, mtawalia.
Jedwali 1: Bei Kikomo za Rejareja (Shilingi/Lita)
Jedwali 2: Bei Kikomo za Jumla (Shilingi/Lita)
Bei za reja reja za bidhaa za mafuta ya petroli kwa maeneo mbalimbali ya miji, wilaya na mikoa ni kama zinavyooneshwa katika Jedwali Na. 3.
Wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa rejareja wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei zinazooneshwa katika Jedwali Na. 3. Aidha, wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa jumla wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei zinazooneshwa katika Jedwali Na. 2. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mfanyabiashara yeyote atakayekiuka AGIZO hili.
EWURA inapenda kuwakumbusha wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta ya petroli kwa jumla na rejareja, pamoja na jamii, kuzingatia yafuatayo:
a) Bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli kwa eneo husika zinapatikana kupitia simu za mkononi kwa kupiga namba *152*00# na kisha kufuata maelekezo. Huduma hii ni bure na inapatikana kupitia mitandao yote ya simu za mkononi hapa nchini.
b) Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, kifungu namba 166, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. EWURA inahamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa hizo.
c) Kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani isipokuwa bei hizo zisizidi bei kikomo (Price cap) au kuwa chini ya bei iliyoruhusiwa (Floor Price) kama zilivyokokotolewa kwa mujibu wa Kanuni za EWURA za Kupanga Bei za Mafuta za Mwaka 2022 zilizotangazwa tarehe 28 Januari 2022 kupitia Gazeti la Serikali Na. 57 na marekebisho ya Kanuni tajwa kupitia Gazeti la Serikali Na. 761A la tarehe 30 Oktoba 2023 na Mabadiliko ya Kanuni za Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja za Mwaka 2024.
d) Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana yakionesha bei za mafuta, punguzo, vivutio vya kibiashara vinavyotolewa na kituo husika. Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta katika vituo vinavyouza mafuta kwa bei nafuu zaidi ili kushamirisha ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja. Adhabu kali itatolewa kwa kituo husika kwa kutotekeleza matakwa ya kisheria kwa mujibu wa kanuni husika.
e) Wauzaji wa bidhaa za mafuta ya petroli wanatakiwa kutoa stakabadhi za mauzo kutoka kwenye Electronic Fiscal Pump Printers (EFPP) na wanunuzi wahakikishe wanapata stakabadhi hizo za malipo zinazoonyesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita. Stakabadhi hizo zitatumika kama ushahidi kwa wanunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo au kuuziwa mafuta yasiyo na kiwango cha ubora unaotakiwa. Stakabadhi hizo pia zitasaidia kurahisisha ukusanyaji wa kodi za Serikali zitokanazo na mauzo ya bidhaa za mafuta ya petroli.

| Bandari | Petroli | Dizeli | Mafuta ya Taa |
| Dar es Salaam | 4,057 | 4,086 | 4,067 |
| Tanga | 4,123 | 4,152 | 4,133 |
| Mtwara | 4,170 | 4,199 | 4,180 |
Jedwali 2: Bei Kikomo za Jumla (Shilingi/Lita)
| Bandari | Petroli | Dizeli | Mafuta ya Taa |
| Dar es Salaam | 3,909.62 | 3,937.91 | 3,920.05 |
| Tanga | 3,906.19 | 3,934.06 | - |
| Mtwara | 3,905.70 | 3,932.94 | - |