Nadhani alitaka akufundishe kitu hapo, ila nadhani kwa utumwa wako kichwani (unatumikishwa kuuamini hata mfumo bora wa kuuishi) uchumi wa fedha, GDP na mavitu kama hayo, alitaka akupe kitu kizuri sana, Kwa mtanzania anaijua vyema nchi yake na mfumo wake wa kuuendesha kwa sera na itikadi zake hawezi kutamani mifumo mingine Kama ya Kenya na India, matajiri wa kupindukia wachache na wimbi la umaskini na maskini katikati yao. Tanzania, ni nchi ya opportunities kwa kila mtu, kila mtu anaweza kuwa yeyote yule, uchumi wa Tanzania kama ungeshamiri kama ilivyotarajia watanzania wangeishi paradiso hapahapa duniani. Ustawi wa kiuchumi si majengo, fedha GDP na mambo kama hayo, hivi ni viashiria tu vya ustawi wa uchumi katu si uchumi au maendeleo yenyewe. Huduma bora za kijamii, chakula chakutosha kwa wote, usawa na haki ktk ajira na fursa haswa ardhi, hapo ndipo patakapotokea ustawi bora wa kiuchumi na jamii kwa ujumla, ndo pakujivunia hapo. Namshangaa mtu anaeshangilia kuwepo ktk dunia ya pili, sijui GDP sijui thamani ya juu ya pesa na mavitu kama hayo wkt raia wengi hawana uwakika wa chakula na si kwakuwa kuna ukame bali hata maeneo ya kulima ni finyu yakihodhiwa na wachache tu, watu wanakufa kwa njaa, eti uchumi umekuwa. Maisha ya waafrika wengi yamedumaha ktk njia hizi za uchumi, eti tumefanikiwa ktk kubadilisha uvaaji, aina ya vyakula, music nk. Maendeleo. Majengo marefu, malls, mabarabara nk, kwa viubongo tulivyoazimishwa. Pole yetu sana wana wa Afrika kwa fikra duni. Kwa IMF na WB mmasai mwenye ng'ombe elfu kumi ni maskini tu kwakuwa hana nyumba ya viwango vyao, nguo zao na chakula cha aina yao,hivyo mwl. mwenye kajumba kamkopo, kapikipiki na vijinguo vya kiwestern vya mitumba kwao ameendelea sana.