Detective J
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 24,058
- 41,518
This is the truth .ifike mahal wanasiasa wetu wa swallow their pride na wakubali kuwa yes.. wanaudhaifu.Suala la kuunganisha magari linaweza lisiwe kubwa LAKINI ukweli ni kuwa katika kipindi hiki cha Uhuru Kenyata, yaliyofanyika, hasa kwenye viwanda, ni vigumu kuamini. Tanzania tunapiga ngonjera majukwaani, Wakenya kweli wanajenga nchi ya viwanda. Ukitaka kufanikiwa, kwanza ukubali mapungufu yako, pili uwatambue waliofanikiwa, na tatu ujitunze kutoka kwa waliofanikiwa. Tunatakiwa kujifunza kutoka kwa hawa majirani zetu.
Nilitembezwa mji wa Kitengela nikaoneshwa viwanda vipya vikubwa na vya kati 32, ilikuwa vigumu sana kuamini. Ukizingatia ukweli kuwa Tanzania kiwanda cha mwisho kikubwa kujenga ni cha Dangote. Kuanzia hapo hakuna hata kimoja kilichojengwa. Tumekuwa wajenzi wa viwanda vikubwa majukwaani visivyoonekana ardhini. Hivyo vya Kenya huhitaji kuambiwa wala kuoneshwa maana vinaonekana wazi, sisi vya kwetu ni zaidi 3,000 lakini kuviona ni lazima uwe mtawala.
Mpatapo nafasi, mnaotembelea Kenya, tembeleeni huo mji ambao miaka ya karibuni ukikuwa mji mdogo sana wa mashamba ya maua, ghafla umekuwa mji wa viwanda.
Maneno mengi vitendo 0.
It time to change kwakweli
Sent using Jamii Forums mobile app