PhD ya Musukuma yazua gumzo, Chuo kilichomtunuku hakitambuliki

Hii udsm sio jalalani au?
 
Yani haya mashada katoka nayo kijijini kwake kuwahi mchongo,kofia utafikiria beseni,ccm kumejaa wajinga tupu
 
Shule ya msingi kasoma kwa miaka 8
 
Udaktari wa Heshima katika Siasa na uongozi, kwa hiyo Sasa hivi tumuite Dr. MSUKUMA[emoji23][emoji23][emoji23]? AFADHARI ya Dr. MAJI MAREFU Udaktari wake aliojitangaza nao ulikuwa unajulikana anafanya nini!
Maji Marefu alikuwa akijiita Prof. Maji Marefu na siyo Dr.
 
Ukiona mwanasiasa kapata PhD au master jua ni ya mchongo.
Hahaha kweli kabisa. Nape, Angela kizigha walisoma pale mzumbe Dar aisee pale ukimpa dr. Barongo sijui prof. Kwa sasa? Ukimpa mpunga unaitwa kwenda kusaini vitabu vyeusi
 
Ninachokifahamu Juu ya American Universal Global Peace (AUGP).
_________
Francis Daudi

Mwaka 2013, Chuo kinachoitwa Academy (au Wakati Mwingine hujiita) American of Universal Global Peace (AUGP) kilizua mtafaruku huko Bangalore, India!

Aliyekuwa Waziri wa Kilimo na Kazi wa Jimbo la Chhattisgarh, Chandrashekhar Sahu alialikwa ili kutunikiwa Udaktari wa Heshima katika Kazi za Kijamii (Social Works). Hii ni kutokana na mchango wake katika maendeleo ya Kilimo na Wakulima! Na kwa Hakika, Sahu alikuwa amefanya kazi nzuri kwenye jimbo hilo lilizungukwa na Vilima.

Sahu akiwa ameshafika Bangalore toka Raiput, hakukuta kinachoitwa Academy of Universal Global Peace (AUGP). Na kibaya zaidi Chuo hiki hakikuwa kinatambuliwa na University Grants Commission(UGC) hii ni kama TCU ya Tanzania.

Mwakilishi wa AUGP alidai Chuo Chao kinatambulika na European Commission, World Peace Organisation na United Nations Global Compact. Hata hivyo iligundulika ni Utapeli Mtupu!

Jambo la kuchekesha ni kuwa, Mwenyekiti wa Academy of Universal Global Peace (AUGP), Dr. Madhu Krishan amekuwa akisafiri na Chuo; Hivyo kimewahi kuwepo Marekani, na Chennai, India!

Kwa bahati mbaya, Chuo hiki sio Christ University(Bangalore) wala International Christian University (Japan). Soma habari hii hapa: Chhattisgarh minister laps up fake honour

Baada ya kisa hiki cha 2013, Wanasiasa wengi wa India walianza kulalama kuwa Mawakala wa American of Universal Global Peace (AUGP) wamekuwa wakiwaomba kati ya Dola (za Marekani) 500 hadi 1,000 ili wapatiwe kinachoitwa "Doctor Honoris Causa"

Kelele zilipokuwa nyingi, hasa utapeli wa kuuza Stashahada: Wao waliandika majibu haya: Ambayo ukichunguza vema utagundua kitu, Rogue academy selling fake honorary doctorate responds to our initial report, accuses C. Hub of wanting to extract huge amount of money from them.

Wakati websites zote za vyuo vya Marekani zina .edu mfano: www.harvard.edu ,
twin-cities.umn.edu hiki Chuo cha Mchongo kinatumia .com yaani augpusa.com na kwa taarifa yako hako ni ka Blogu tu kwenye WordPress. Umeelewa? Ifungue kisha nenda hadi mwisho utaona!!

Mwisho: University Nations (UNU) University kilitangaza kwenye website yake kuwa hakina uhusiano wala ushirikiano na hiki kinachojiita American University of Global Peace!! Soma hapa: False claims of affiliation with UNU - United Nations University

Ni muhimu kabla haujatunukiwa Udaktari wa Heshima ukachunguza haya!

Francis Daudi.
 
Mimi namthamini kila mtu kwa jinsi Mungu alivyomjalia na si kwa sababu ya pesa maana ni pesa zake na si zangu na sina mgao kwa pesa zake. Katika jamii tunaishi kwa kutegemeana - mwenye pesa anamtegemea mtu mwingine asiye na pesa kwa kitu au jambo alilo na shida nalo. Mfano, mwenye pesa akiumwa jino ataenda kwa dentist, ambaye hata hajajenga nyumba, hana gari, lakini anaweza kumtibu. Watoto wa mwenye pesa atawapeleka shule au kwa baadhi ya wenye pesa atawanyima elimu ya shule na kuwapa mali. Lakini kuwa na mali hakuondoi umuhimu wa elimu kwa mwanadamu. Heri uwe na pesa na uwe umesoma kuliko kuwa na pesa na uwe hujasoma au huna elimu ya darasani.
 
Kwani ina tofauti gani na ya Jaffo?
Haya, kuna ile PhD ya Magufuli nayo ilizua mjadala, ambao ulizimwa baada ya mpingaji mkuu wa PhD hiyo kupotezwa jadi leo. Ben Saanane. Ya Jaffo sijaifuatilia binafsi, lakini tunaweza kuorodhesha hapa PhD zenye utata:
1) Dr. Magufuli
2) Dr. Msukuma Kasheku
3) Dr. Jaffo
Hivi ile ya Lyatonga Mrema ilikiwa ni Bachelors au Masters au PhD? maana watanzania kwa digirii za kuchonga tu hatujambo
 
Na wewe unauliza?
Prof Jay mjumbe wa kamati kuu ya Chadema

Ndiye Prof pekee pale Ufipa kwa sasa!
Umewahi kumsikia Profesa J katunukiwa PhD? Au uprofesa? Yeye kaamua tu kujiita kutokana na usanii wake. Hakuwahi kuvaa magwanda ya graduu ya chuo kikuu kama huyo msukuma.
PhD ya Msukuma ni kituko cha pekee, acha kulazimisha wa "kufanana na" Msukuma
 
Taarifa yako haiko sawa. Msukuma hakupewa PhD bali Doctorate pamoja na kwamba ni ya kuchonga.
 
Eti anaitwa dr Msukuma KWa Sasa, ila sawa mbona tulishakua na prof maji marefu,
 
Yote haya yanachanzo chake wenyewe wenye chama wanajui sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…