Aisee wanasiasa mnakatisha watu tamaa ya kusoma bhana, watu wanahangaika kusoma kwa taabu wanakesha usiku, Kuna wengine Familia zinauza Mali za ukoo ili kijana asome, wengine wa nashindwa kumaliza kwa kukosa Ada na wengine wanashindwa kwa kufeli mitihani(discontinuation).
Masikini ya Mungu na wengine watoto wa kike mpaka wanauza utu wao kwa waalimu wao kwa kutoa rushwa ya ngono, halafu huku nyie yaani mnapeanapeana tu, eti mara Degree ya heshima, mara PhD ya heshima, acheni mzaha na elimu jamani, Elimu ni IBADA.