Philip Mangula ang'atuka nafasi ya Umakamu Mwenyekiti CCM Taifa. Abdulrahman Kinana apendekezwa na Halmashauri Kuu kuchukua nafasi yake

Basi nyie safu mpya,mtukumbuke huku mtaani Hali Ni mbaya sana
 
Mwenyekiti - samia suluhu hassan
makamu mwenyekiti/bara - Abdulrahmani kinana
makamu m/kiti visiwani - hussein ally mwinyi/ally mohamed shain
Katibu mwenezi shaka hamdu shaka
Katibu mkuu - Daniel chongolo
Naibu katibu mkuu Alhaji ?????
Yaani wapwani watupu wamejazana.Nchi hii iko kwa shetani haswa.
 
Kwenye uongozi kuna wakati sio rahisi kuelewana itikadi, na hii inatokea pale unapohudumia awamu zaidi ya moja kwa Viongozi wakuu tofauti. Ngoja mzee akapumzike
Kwani "itikadi" ni nini mkuu?

Ina maana "itikadi" ni ya mtu/kiongozi na siyo ya chama au siyo?

Kwa hali ilivyo sasa ndani ya CCM ninakubaliana na wewe moja kwa moja, kwa sababu Magufuli alileta itikadi yake, wakati Makamu wake akiwa Samia, akakubali kufanya kazi kutekeleza itikadi hiyo. Magufuli "alipong'atuka", makamu wake Samia naye katanguliza "itikadi" yake!
Sasa, kama unayosema ni kweli, inakuwaje Mangula atoswe?

Huenda ikawa vigumu kwako kuelewa ninachoeleza hapa.
 
Recycling old tired stuffs. CCM kwa sasa hakina maono, umakini, utashi, mikakati ya kusaidia na kuwazesha Watanzania.
CCM ni ile ile, Je lini ilikuwa Tofauti?
Your browser is not able to display this video.
 
huyu Bwana aliachwa kipindi cha Kikwete. Si mzungumzaji sana. ni mtu mkimya asiyependa makeke.. ila wanasema ni mwenye msimamo sana. alipoachwa/acha nafasi ya ukatibu mkuu akarudi zake Iringa kwenda Kulima.... akawa Mkulima humsikii.. Alipokuja Magufuli akaenda mchukua huko Iringa... akawa naye katika Uongozi... zikaja habari za kuwa aliwekewa sumu....
1. nani alitaka kumuua?
2. kwa nini?

amekuja Samia Suluhu ni wazi ameona amrudishe Kinana ambaye alikuwepo wakati wa Kikwete ... huyu ni Mzee wa Meno ya Ndovu. ni mtu poa sana. mi nimefurahi kurudishwa kundini.

JE NINI UKWELI KUHUSIANA NA MANGULA. KUNA NINI NYUMA YAKE?
 
Siyo 10 huyu mzee pia alikuwa Vice Chairman kwa Marehemu Mkapa ni hazina ambayo Ccm yenyewe inamtegemea kiukweli,japo yule Nyoka (Shetani) alitakaga kumuuma mzee wa Watu🤣🤣🤣🤣
kwa Mkapa alikuwa katibu mkuu kwa miaka 10.
 

Ila utakuwa umesahau mambo kumhusu mzee Mangula. Iringa hakutulia bali aligombea kila cheo huko hadi balozi nyumba kumi. Vyeo vyeto hivyo aliliwa kichwa na wanaume.

Huyo ndiye mzee Mangula aliyepewa sumu kwenye songombingo la kuwala vichwa kina Kinana.
 
oohh...issue ilikuwa ni hawa hawa akina kinana? ndo wamerudishwa tena kuchukua nafasi yake? hizi siasa zina mambo yake aiseeeeeee
 

Kwa zile siasa za kihanithi alizoleta dhalimu, acha hayo majizi ya msoga yarejee. Nani anamsifia huyo mama, sisi tunashukuru nchi hii haiongozwi kwa siasa za kihayawani. Ccm haitegemei kura kukaa madarakani, na dhalimu ndio alikoleza tabia hiyo. Na hiyo ,2025 haitashinda kirahisi maana haina ushawishi wowote zaidi ya kutegemea vyombo vya dola. Cha muhimu dhalimu hayuko madarakani.
 
Mangula aliwahi kutolewa kwenye nafasi hiyo, baadae Tena wakaenda kumuangukia arudi.
Kwahiyo Mangula hatakiwi kustaafu. Ni mpaka AFIE madarakani?

Hii NCHI, wanasiasa Ni tatizo. Ila wafuasi wa wanasiasa wote Ni tatizo kubwa mnoo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…