Philip Mangula ang'atuka nafasi ya Umakamu Mwenyekiti CCM Taifa. Abdulrahman Kinana apendekezwa na Halmashauri Kuu kuchukua nafasi yake

Lile tamasha la kumbukizi ya kifo cha hayati Moses Nnauye pale Diamond Jubilee lilikuwa linatuma ujumbe mzito sana...kumbuka waliokuwa wasemaji wakuu.....
KILE KILIKUWA KIKAO MAALUM NA SI TAMASHA..ILIKUWA NI NGUMU KWA WAO KUKUTANA PAMOJA KM VILE
 
Mangula alichoshwa na fitina akaachia ngazi.
Ccm walipoona mambo mazito walikwenda kumpigia magoti akiwa ameanza kuwa mkulima.

Huu ni muhimili muhimu sana cxm.
Mzee hanaga maneno mengi lakini ni bwana mikakati mzuri sana.
 
Afadhali!
Alikuwa hafanani nao hata kidogo.
 
Miaka 81 amelitumikia taifa kwa kutukuka
Niko shule ya Msingi nasoma darasa la 5, Mh. Mangula alikuwa Mkuu wa Wilaya yetu ya Kwimba na tuliwahi kumwalika kwenye kata yetu kama mgeni rasmi kwenye sikukuu ya Sabasaba. Alikuja akiwa amevaa kombati za JWTZ. Wengi wasichokijua ni kwamba Mangula pia ni mwanajeshi wa JWTZ, ila wengi hawajui hilo
 
Dkt Bashiru sijui anajisikiaje hapo alipo. Kwani wale aliowatuhumu kuwa walikuwa ni wabadhirifu na kujitwalia kiholela mali za chama ndiyo hao hao sasa wanarudishwa katika nafasi nyeti ndani ya chama na kuwa ndiyo mabosi zake.

Zoezi alilolisimamia la kuhakiki mali za chama sasa linageuka kuwa shubiri kwake. Wale waliodukuliwa wakimteta na kumsimanga "the big boss" inadhihirisha sasa kuwa walikuwa na hoja za msingi za kufanya hivyo.

Kweli dunia ni hadaa na ulimwengu ni shujaa.
 
Sera za kuhamasisha uhai wa chama kwa kutumia ubwabwa na magharagwe zarudi kwa kasi ya kazi iendelee . Muda si mrefu Mungu ataonesha Neema yake juu ya Tanzania atanyanyua mawe ya tetee wanyonge na maskini wa Taifa hili.
 
Ma Rais wote wakikabidhiwa chama hubadili Katibu Mkuu, hata Mkapa alibadili, hata Mwinyi alimuweka Horace Kolimba…iweje mlitazamia Jk aendelee na Mangula kwny Ukatibu Mkuu?

Timu Msoga wanarudia ya 2005 kumuondoa Mzee Mangula,Maji yalipozidi unga JK ikabidi amtafute Mzee Mangula.Mama naona kama amezidiwa kete na Msoga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…