Nashukuru kwa kunitusi kuwa mimi ni mbumbumbu.
ila umbumbumbu wangu umenionyesha hivi.
Kagame anawasupport M23 na inaonekana ,sehemu kubwa ya M23 ni wanajeshi wa Rwanda waliojificha ndani ya kivuli cha M23.Rwanda na Uganda wamekuwa wakiiba sehemu kubwa ya Rasilimali za DRC kupitia wanajeshi wao.Na ndio maana Miongoni mwa watu wenye hela nyingi Rwanda ni wanajeshi.Kikwete aliona mbali sana uhuni wa mikutano ya usuluhishi,kuwa ni kiini macho, na ndio maana kwa kushirikiana na SADC wakaomba UN wawaruhusu kusimamia vikosi vya kulinda amani DRC,Hapo ndipo chuki halisi ya Kagame kwa kikwete ilipoanza, kwani Kagame alijua fika kwamba kitumbua chake kinaingia mchanga.Ndio maana toka SADC ilipoamua kuingia hapo,kila mtu alikua akilalamikia Tanzania ,kwanini ipeleke majeshi yake,hawakuzungumzia majeshi mengine,kwani wanatujua vyema.
Hivyo basi kauli aliyoitoa Kagame ya kumdharau JK,haitokani na ukweli kwamba ule ushauri ni mbaya,ila ilikua kauli ya chuki kutokana na JK kupeleka majeshi DRC ambapo KG,amekua akiiba rasilimali kule.Sasa kinachotokea,Uchumi wa Rwanda hautakua tena kwa kasi ile waliyojisifia na ndio maana kwenye hii EAC wanapoitenga Tz,wanajaribu kuua sehemu ambazo wanajua ,zinaendesha uchumi wa TZ ,ili nao kutukomoa,kwamba "wewe mwaga mboga, na mie namwaga ugali"
Lakini soon itathibitika Rasmi kwamba Kagame na Museveni ndio M23.Itakua hivi,M23 saa hizi wanapigwa,mwisho wa siku ni lazima tu watakimbilia kule wanakotoka,nako si kwingine ni Rwanda na uganda.na sehemu kubwa itakua ni lazima Rwanda.sasa majeshi haya ya kulinda amani ni lazima yaingie huko kuwa maliza.Kitakachotokea ni nini/rwanda itaanza kulalamika kwamba majeshi haya yameingilia Rwanda ili kutafuta sababu ya kuyapiga.Na ndio maana propaganda zimeanza mapema,za kujifanya oooh,mabomu yanarushwa rwanda toka DRC kumbe ni uongo,mabomu yanapigwa toka Rwanda.
Hili tuliishaliona mapema pale Kagame alipoanza kupanga upya safu yake ya kijeshi.Kwani ameishaanza kujiandaa kupambana.
Mwisho wa siku ,siku zenu zinahesabika,nawaoneeni huruma sana.waulize M23, kinachoendelea huko.Kiufupi nyie ni watu wanafiki sana.Na jumuiya ya kimataifa inajua kwamba nyie ndio mnafanya amani DRC isiwepo.Na ndio maana Tanzania ilikataa msiingie EAC mpaka mmalize migogoro yenu kwanza.Mkatetewa na Mseveni,wenu mkisema matatizo ya vita yataisha kirahisi mkiwa ndai ya EAC,kumbe mlikua mnatafuta chaka la kujifichia.Matokeo yake mmetoka na migogoro yenu huko mnakuja kutuletea na sisi.
Lakini hili pia ni fundisho kwa Tanzania kwamba dunia ya sasa haina kitu cha bure.Watu hawa tumewafadhili sana,na wengi wao tumewasomesha bure na wengine wamefanya hata kazi kwenye taasisi zetu,tukaacha hata kuwasomesha vijana wetu,na pia tumewasaidia sana akiwemo Kagame mwenyewe,matokeo yake ,yeye ndio anatudharau na kujifanya kiburi.Ni wakati sasa wa kuanza kulipwa kwa kile tunachokifanya.Kwa mf' ni wakati hata wa DRC kuanza kuangalia,baada ya UN mission kuisha,tutakapoisadia kuanza kutrain vijana wao,itulipe ili kuachana na mambo ya tenda wema nenda zako.Mataifa yote makubwa Duniani hayakusaidii bure.
Huo ndio umbumbumbu wangu kwa leo.
DUH KWELI HUNA KAZI YA KUFANYA UNAWEZAJE KUANDIKA UTUMBO MREFU KIASI HIKI BILA HATA YA KUJISTUKIA...UNAJUA KONGO YAPO MAKUNDI MANGAPI YA WAASI ZAIDI YA M23?hakuna unachojua zaidi ni hisia tu na stori mnazolishana kwenye vijiwe vya kahawa na unga...."kwani wanatujua vyema" unachekesha sana...huwezi ukajifunza wenzako wanafanyaje kama ukiwa na mawazo mgando kama hayo....kiboko yetu watz ni Berth 19 iliyokuwa commissioned leo....ni kwasababu ya slugishness ya ubongo wenu ndo maana hamuwezi enda kwa speed ya eac...fuatilia speech za leo mombasa za marais 3 Kagame,mseven,uhuru...unadhani nani ana haki miliki ya eac?mi kama raia wa tanzania si afiki mawazo yako juu ya sakata la congo...ila kwa kuwa tumezoea zidum fikra za mtu flani ndo maana wenye fikra tofauti mnatuita wanyarwanda.....
rwanda inajua vita ni nini ndo maana piga ua haiwezi ingia vitani hta kidogo...ila kwa sababu tumerithi amani hatujui thamani yake ndo maana tunashabkia vita....keep knowing "vita kati ya nchi na nchi si sawa na mechi ya mpira kati ya timu ya taifa na taifa"
CHA MAANA NI KUJITAHIDI KUITUNZA AMANI TULIORITHI.....MUNGU IBARIKI AFRIKA MASHARIKI





