Picha adimu ya Mwalimu Nyerere 1950s

Picha adimu ya Mwalimu Nyerere 1950s

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
MOJA YA PICHA ADIMU ZA BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE

Iko siku miaka michache iliyopita nilikwenda kumtembelea nyumbani kwake Magomeni Mikumi Kisiwani, rafiki yangu toka udogoni Maulidi ''Chubby'' Tosiri.

Nilikuwa na taarifa kuwa alikuwa mgonjwa.

Basi katika mazungumzo yetu Chubby akanyanyuka akaingia chumbani kwake akaja na picha kutoka kumbukumbu za baba yake Mzee Iddi Tosiri.

Mzee Tosiri ni kati ya watu wa mwanzo kujiunga na TANU na kujuana na Julius Nyerere.

Iddi Tosiri na Iddi Faiz Mafungo ambae sasa naamini si mgeni kwa wasomaji wangu ni ndugu na Sheikh Mohamed Ramia.

Sheikh Ramia kwao wao ni kaka yao binamu. Iddi Faiz na Iddi Tosiri ndiyo waliyomchukua Mwalimu Nyerere mwaka wa 1954 kwendanae Bagamoyo kumjulisha kwa Sheikh Mohamed Ramiyya.

Chubby alinipa picha kadhaa adimu akiwemo baba yake Mzee Tosiri na Mwalimu Nyerere wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Ukisikia historia hizi na ukaona na picha lazima mwili utakusisimka.

Iddi Faizi anadamka alfajir kutoka nyumbani kwake Ilala anampitia Iddi Tosiri nyumbani kwake Mtaa wa Livingstone kisha wanakwenda ofisi ya TANU New Street ambako si mbali na nyumbani kwa Iddi Tosiri.

Pale wanamkuta Mwalimu Nyerere keshafika zamani anawasubiri.

Wanatoka hapo kuelekea Soko la Kariakoo kupanda basi la Bagamoyo.

Kila unaposikia historia hizi zikihadithiwa unataka anaeeleza asiache kuzungumza.

Rafiki yangu Chubby baada ya kunipa picha hizi hakuishi sana baada ya muda akafariki dunia.

Picha hizi alizonitunuku zimekuwa kama zawadi kwangu kutoka kwake na kutoka kwa baba zake wote watatatu - Iddi Tosiri, Iddi Faiz na Sheikh Mohamed Ramia.

Nimeona leo niweke hapa Barzani moja ya picha hizi kama kumbukumbu ya sahib yangu Chubby na pia kama kukumbuka ya historia ya wazee wetu na Baba wa Taifa wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika:

JULIUS NYERERE NA MIKUKI.jpeg
 
Naona hapo umeandika "picha hizi alizonitunuku" lakini picha uliyoiweka ni moja.
 
Hivi Taifa limewapa nafasi watoto wa hao wazee waliopigania uhuru,?
Kizazi chao ilibidi kiwe ndani ya systems, jeshini, waizarani, kwenye balozi, ndani ya siasa
 
Nyerere alikataa kujenga taifa lenye matabaka ya mabwana na watwana.

Ndiyo maana hata uchifu aliukataa.

Angefanya hivyo ukivyooendekeza, angekuwa kajenga jamii yenye matabakq, kungekuwa na tabaka la watu waliowahi kujiunga TANU mwanzo na kupigania Uhuru, na tabaka la wengine.

Nyerere kama mjamaa, hakuamini katika kujenga jamii yenye matabaka.
 
Hii nayo ni myth tu
Data zinaonesha hadi anastaafu wakatoliki
Ndo walikuwa kama Tabaka la watawala hapa nchini..

Foundation aliyoiweka imefanya hadi
Non Catholic iwe ngumu kutoa Rais..
Three Christians President both Catholic na imetokea Tu by accident?

Kanisa Catholic kumtangaza mtakatifu mtu
Allegedly 'mjamaa 'nayo imetokea tu?

Now Rais wa maisha mtarajiwa kuna siku
Atatangazwa 'Mwenyeheri'kama Nyerere
Na watu wataona 'imetokea' tu..

Mwandosya -moravian
Lowasa -KKT
Membe -KKT.

Now ni ajali aliepitishwa third time alikuwa
RC? I don't think so

Dr Slaa ,Mwanakijiji both now wame team up
Na their fellow Catholic nayo 'imetokea' tu?

Hapana ...hakunaga accident Kwenye politics.
 
We jamaa akili zako nowadays zinafikirisha sana, huo udini utakumaliza.
 
Back
Top Bottom