Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
MOJA YA PICHA ADIMU ZA BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE
Iko siku miaka michache iliyopita nilikwenda kumtembelea nyumbani kwake Magomeni Mikumi Kisiwani, rafiki yangu toka udogoni Maulidi ''Chubby'' Tosiri.
Nilikuwa na taarifa kuwa alikuwa mgonjwa.
Basi katika mazungumzo yetu Chubby akanyanyuka akaingia chumbani kwake akaja na picha kutoka kumbukumbu za baba yake Mzee Iddi Tosiri.
Mzee Tosiri ni kati ya watu wa mwanzo kujiunga na TANU na kujuana na Julius Nyerere.
Iddi Tosiri na Iddi Faiz Mafungo ambae sasa naamini si mgeni kwa wasomaji wangu ni ndugu na Sheikh Mohamed Ramia.
Sheikh Ramia kwao wao ni kaka yao binamu. Iddi Faiz na Iddi Tosiri ndiyo waliyomchukua Mwalimu Nyerere mwaka wa 1954 kwendanae Bagamoyo kumjulisha kwa Sheikh Mohamed Ramiyya.
Chubby alinipa picha kadhaa adimu akiwemo baba yake Mzee Tosiri na Mwalimu Nyerere wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.
Ukisikia historia hizi na ukaona na picha lazima mwili utakusisimka.
Iddi Faizi anadamka alfajir kutoka nyumbani kwake Ilala anampitia Iddi Tosiri nyumbani kwake Mtaa wa Livingstone kisha wanakwenda ofisi ya TANU New Street ambako si mbali na nyumbani kwa Iddi Tosiri.
Pale wanamkuta Mwalimu Nyerere keshafika zamani anawasubiri.
Wanatoka hapo kuelekea Soko la Kariakoo kupanda basi la Bagamoyo.
Kila unaposikia historia hizi zikihadithiwa unataka anaeeleza asiache kuzungumza.
Rafiki yangu Chubby baada ya kunipa picha hizi hakuishi sana baada ya muda akafariki dunia.
Picha hizi alizonitunuku zimekuwa kama zawadi kwangu kutoka kwake na kutoka kwa baba zake wote watatatu - Iddi Tosiri, Iddi Faiz na Sheikh Mohamed Ramia.
Nimeona leo niweke hapa Barzani moja ya picha hizi kama kumbukumbu ya sahib yangu Chubby na pia kama kukumbuka ya historia ya wazee wetu na Baba wa Taifa wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika: