Hata watoto wameruhusiwa kushiriki shughuli za kampeni za uchaguzi?Leo pale Kinyerezi DSM nimewashuhudia watoto wadogo wakiwa jukwaani na wasanii,Mh.Mgombea wa CCM alipanda jukwaani na kucheza nao/kuwatuza.Je,sheria inawaruhusu kushiriki mambo hayo kabla ya hata kujadili suala la kwa nini hawapo shule ilhali leo ni Jumatatu?Kimaadili hili ilmekaaje?
Hizi kampeni za watawala kila siku zinasababisha sana uvunjifu wa maadili na Katiba/sheria za nchi ila hatua hazichukuliwi ipasavyo,kuna wagombea kama haki ingekuwepo walistahili kuenguliwa kwenye kinyang'anyiro kitambo sana.Watanzania inabidi tupige kura za kimbunga ili wezi washindwe kuiba kura zetu,tuzilinde na tutangaziwe washindi halali tu,Amen.