Picha: Bweni lililomliza Naibu Waziri Mahiza Tanga

Picha: Bweni lililomliza Naibu Waziri Mahiza Tanga

Mungu wangu! Sijawahi ona maishani mwangu! Ee Mungu tunusuru viumbe wako.

Unaweza kutokwa na machozi. Pamoja na utajiri mkubwa wa rasilimali tulizonazo ikiwemo Dhahabu, Alamasi, Tanzanet, Uranium, Misitu, Vivutio vya mbuga za wanyama lakini prioruties za viongozi wetu mafisadi ni kujitajirisha wao na vibaraka vyao mapapa mafisadi. Hali kama hii ya Tanga si ya pekee katika nchi yetu bali ziko mahali mbali mbali katika mikoa yetu. Halafu bado kuna wapuuzi wanataka Kikwete aendelee mpaka 2015 pamoja na kuwa kuna ushahidi wa kutosha kwamba ameshindwa kabisa kuongoza nchi katika kila nyanja. Mungu ibariki Tanzania.
 
At least something alternative to MENGI vs ROSTAM episodes


btw kule Mbagala hali inazidi kuwa mbaya apparently wamekufa wanajeshi wengi kuliko tunavyoambiwa

kuna thread ya Hussein Mwinyi sijui iko wapi nimejaribu kuisearch lakini wapi!!

mtu pekee ambaye amefikiria habari ya Mengi na Rostam kwenye mada hii ni wewe. Usingeweza kufanya vinginevyo. Wengine tunafikiria na mambo mengine.
 
Na sisi tunasema tupo karne ya 21 ya sayansi na Tekinologia???..................KWELI

Wabunge wetu wanataka kujiongezea Mishahara na Marupurupu wkt wapi kura wao hawana Bweni.....................Kweli Tumerogwa na Mganga aliyeturoga ameshakufa
 
Bweni lenyewe hili hapa. Inasikitisha sana

Is this true au mnachapia tu? Siamini kwamba hilo ni bweni ambalo wanafunzi wanapashwa kuwa wanaishi. Hiyo wilaya ina afisa elimu, na wa mkoa pia yupo na wanaona hiyo hali ni sawa? Then kuna tatizo mahali!!!!!

Nashindwa kuamini.

Tiba
 
Mungu wangu! Sijawahi ona maishani mwangu! Ee Mungu tunusuru viumbe wako.

Huko tuliko ibukia wengine hayo maisha ni ya kawaida kabisa mkuu......tunalalamika tukiwa tulishafeel ugumu wa maisha huko bush mkuu! Haya yanatakiwa kubadilishwa na sisi now na kuyafanya historia!
 
Huenda analia kuwa kwenda huko kuomba kura 2010 itakuwa mbinde kwani kutegemea nafasi ya viti maalumu ni ishu. Kumbe ni ALUMNI wa Zingibari!
Labda machozi yalimtoka kwa sababu: (1) Kura 2010 (2) Kuumia nafsi kuwa amekaa mbali na wanakijiji wenzie, jamii na marafiki hata kupata aibu ya kupita kiasi.

Lakini, hii ndio shule pekee yenye hali hii? yeye kama naibu mwenye dhamana ya wizara husika anatakwimu zinazoonyesha hali ya makazi ya wanafunzi katika taasisi mbalimbali za elimu zilizopo chini yake? Huyu analia kisiasa, wakati nia yao ni kuona wananchi wanabaki hivyo wasije kujua mbele wala nyuma, wasiwe na umeme, TV wala uwezo wa kununua magazeti ili wasije kujua ukweli wakawanyima kura (nukuu: Mkuchika)!
Profile yake!

Salutation: Honourable
First Name: Mwantumu
Middle Name: Bakari
Last Name:Mahiza
Member Type:Special Seat
Constituent:No Constituency
Political Party:CHAMA CHA MAPINDUZI
Office Location:P.O.Box 9121, Dar es Salaam

EDUCATIONS School Name/Location Course/Degree/Award Start Date End Date Level
Chang'ombe Teaching Training College Diploma 1986-1987 DIPLOMA
Korogwe Teaching Training College Certificate 1971- 1972 CERTIFICATE
University of Oslo - Norway Teaching Course 1990- 1990 DIPLOMA
Jerusalem College - Israel Curriculum Development Course 1997 - 1997 DIPLOMA
Beit Bel Teaching College - Israel Teaching College 1999- 1999 DIPLOMA
EDEPA University College - New Delhi, India Diploma in Teaching, Admin & Management 2000 -2000 DIPLOMA
Korogwe Secondary Secondary School Secondary Education 1967- 1970 SECONDARY
Zingibari Primary School Primary Education 1962-1966 CERTIFICATE
 
wengi wanaweka hizi priority kwanza , hawajui hali halisi au ndio wanachukulia DSM kama ndio Tanzania, pili wamejaa choyo na ubinafsi, tatu hawana uzalendo kwa taifa hivyo hawajui lipi la muhimu na lipi si la muhimu. Hata huyu waziri katu asingetoka machozi kama asingetembelea huko!

Wanaijua sana hali halisi, tena sana tu, ila hawaweki vipaumbele kwa maslahi ya taifa bali kwa maslahi yao binafsi. Mradi wa vitambulisho vya uraia ambavyo utakaogharimu mabilioni ya pesa si kipaumbele chetu kwa sasa! Na wao wanalijua sana hilo...Lakini kwa kuwa kuna maslahi binafsi ya kujineemesha wao na familia zao, wanang'ang'ania mradi huo uanze mara moja!

Wizi mtupu!
 
Naomba niwe MKOROFI.

Hapa UZEMBE unaanzia kwa:-

1. Wanafunzi wenyewe. Mtakaaje kwenye jengo bovu namna hiyo na nyie mnakubaliana na hali hiyo? Yaani hapa unaona ni kwa jinsi gani Watanzania ni Wazembe wa kufikiri. Unakaa kusubiri hadi Mkuu wa Nchi wa Nchi au sijui nani aje akujengee. Hata kuchukua Makuti na kuezeka hapo juu nalo ni tatizo? Mwisho wa siku wanaoumia ni wenyewe wanafunzi. Na ukiangalia hilo njemba limesimama nje ya bweni na PEDESHEE yake, huwezi amini humo ndani anaishi.
Hii inanikumbusha tulipokuwa JKT Msange (1989-1990), alikuja Makame na kukuta watu wanawasha kikoroboi ambacho ni Domitory Made. Akauliza kama kuna redio, akajiiwa hamna. Akatukana sana sana na hadi niliamini siku hiyo kuwa kweli INABIDI KUKIBADILISHA kizazi hiki hata ikibidi kwa VIBOKO ili watu waanze kufikiria na si kufanya kwa MAZOEA. Akasema, kwa nini tunashindwa hata kutengeneza Mkaa na kuuza mjini na kununua hivyo vitu. Basi kabla ya mwezi kufika, kila company ilikuwa na Redio na taa za karabai kwa hela ya Mkaa. Nakumbuka hotuba ya Nyerere kuhusu vyama vingi niliisikia kwa kutumia redio hiyo. Mpira wa Argentina na Cameroon (0-1) tulisikia matokeo kupitia redio Burundi na Waha wakawa wanatafasiri nini kinasemwa.

2. Kama hapo juu, Waalimu pia nawaunganisha. Ila sitashangaa kwani waalimu wa sasa si ndiyo sisi ambao hata kufikiria kuwa na kiredio tulikuwa hatujui? Mnyororo wa Kizazi kilichooza unazidi kuendelea. Sasa sijui nini kitatokea hawa vijana wakijakuwa nao eti WAALIMU au MAWAZIRI.

3. Wazazi wao pia nawajumlisha. Ila kutokana na mazingira ambayo wazazi wanaishi, hawa sintawalaumu sana.

4. Viongozi wa Chama na Serikali kuanzia chini hadi huko juu na hapo changanya na mama mmwaga chozi. Hawa wanatengeneza KIZAZI kibaya kuliko vyote ambavyo vimeshawahi kuwepo Tanzania. Mtu anafikiri kwa sababu yeye watoto wake wanasoma shule nzuri basi hili halimhusu. Ila inawezekana huyo jamaa kwenye picha ndiyo anaweza kuja kuwa Daktari wa Muhimbili. Sijui product gani itakuwepo hapo.

Hili ni JIPU. Ili kulipasua, inabidi kutomwangalia mgonjwa usoni. Mtu aje na maguvu yake bila kujali haki za binadamu na ALIPASUE HILI JIPU.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.

NB: ELIMU YA KUJITEGEMEA ILIFIA WAPI???????
 
Inasikitisha.
Hilo ni bweni au kichaka?

Ndo bweni eti mpaka huruma. Kama Mahiza amelia hao watoto wanafanyaje? Kulia lia tu,kama kahuzunishwa then abadilishe kuwa furaha. Msaada au usimamizi autoe ili waweze kujengewa bweni ambalo binadamu aanaweza kuishi kwa amani,usalama,usafi na furaha.
 
national examinations council of tanzania

csee 2008 examination results

s0907 zingibari secondary school

div-i = 0 div-ii = 2 div-iii = 15 div-iv = 56 fld = 7 abs = 1
 
Last edited:
At least something alternative to MENGI vs ROSTAM episodes


btw kule Mbagala hali inazidi kuwa mbaya apparently wamekufa wanajeshi wengi kuliko tunavyoambiwa

kuna thread ya Hussein Mwinyi sijui iko wapi nimejaribu kuisearch lakini wapi!!

Mkuu yaani na wewe ulitegemea kabisa serikali ya bongo ikupe accurate figures? Yaani kabla hawajasema wangapi wamekufa nilijua ili kupata accurate figure chukua hiyo namba wanayokupa halafu tafuta square yake!


At the risk of blaming the victim, hao wanafunzi nao wana lawama kwa kukubali kulala katika hilo bweni.
 
rmashauri said:
div-i = 0 div-ii = 2 div-iii = 15 div-iv = 56 fld = 7 abs = 1

..madogo waliochana div II katika mazingira kama hayo wanastahili pongezi.

 
Hii haiwezi kuisha bila ya watu kusikiliza tena wimbo wa Mpoto na Banana wa nikipata nauli/Mjomba. Aliyoimba na ukiangalia lile bweni, utafikiri alishaliona hili bweni. Bahati mbaya hakuliweka hili jengo ndani ya hiyo Clip.

[ame=http://www.youtube.com/watch?v=aiuEmI2i2rw]YouTube - MPOTO feat BANANA nikipata nauli (www.nahoza.ning.com)[/ame]
 
Chakushangaza mawaziri wetu walipita kwenye shule kama hizo hizo pekupeku! Leo hii wana foreign bank accounts....inaumiza kichwa! Sasa jamani kwa hesabu za fasta fasta the price of a brand new toyota landcruiser vx 2008 model..mabweni ya tofali yenye madirisha na umeme maji mangapi????
Tumelogwa au? Mbona kujipatia umaarufu kwenye siasa ni kazi ndogo sana jamani...ata kama umwekwapua bot jenga shule 7 za kisasa jimboni kwako.. , weka umeme, tengeneza barabara vuta maji....
Ilani ya ccm inakataza kuendeleza majimbo au?? coz most mps can easily afford to bring maendeleo vp??
 
Tunaweza kusema yote lakini kama wananchi hatuamui huduma za kijamii ziendeshwe na mrengo wa kushoto ama kulia basi tutaendelea kuyumbayumba tu hapo kati.

Kilichomfanya waziri kulia ni nini? Je ni imani ya utu ama ni utambuzi kwamba watanzania hawana haki za msingi katika taifa lao?
 
Mzee Mwanakiji,

Mie nimesikitisha sana alafu watu kama hawa utasikia wanasema wanaenda Vacation,yaani with our money?


DSC_6836.jpg
DSC_6836.jpg

Vipaumbele vya tifa letu ni vipi?..Mie wakati mwingine huwa najiuliza tunaenda wapi?
 
Last edited:
Back
Top Bottom