Sijui nini kimevikumba vyombo vya habari Tanzania.Sijui ni ulimbukeni,sijui ni hofu ya kutumbuliwa hasa wakurugenzi wateule,au nini sijui!
Hii Channel ya utalii ilianza vizuri sana. Nilitegemea ijikite kwenye maudhui halisi ya utalii pekee. Cha ajabu kadri siku zinavyosonga inageuka kuwa chanell ya kuonyesha miradi ya Serikali kama Stiglers n.k. Kwani habari kama hizo si ndio kutwa nzima zinaonyeshwa pale TBC1 na Channel Ten? Kwanini mnalazimisha kutupa habari tusizozitaka? Sasa kulikuwa na maana gani ya kuanzisha Safari Channel kama hamna maudhui?
Tanzania ina mambo mengi sana ya kitalii ambayo mtu huwezi kuyamaliza ndani ya miaka 3. Shida ni Management ya TBC kugeuza vyombo vyake vyote kuwa "Praise Team" mpaka mnaharibu. Kusifia kumezidi mpaka wanaotutazama wanatuona washamba. Hebu fikiria mtu wa nje ya nchi ana tune Safari Channel aafu ghafla anakuta kada anahojiwa miradi ya serikali je atarudia tena kutazama?
Primary purpose ya kuanzisha Safari Channel ilikuwa kuwavutia watalii wa nje kuja kufanya utalii nchini na si kuitumia kwa propaganda za kisiasa.Hali ikiendelea hivi baada ya miaka 10 ijayo tutaanza kuona mikutano ya chama ilirushwa live kupitia hii Channel.