nakumbuka kipindi cha nyuma bado bwa'mdogo tulikuwa tunaenda kucheza baharini, Unaweza kutembea hata zaidi ya mita 50kwenye maji kuelekea kina kirefu ndio maji yakufike kifuani au mabegani, hapo tunasubiri mawimbi makubwa kama haya unayoyazungumzia linapokuja kwa nguvu unajirusha katikati(mchomo)basi linakubeba kwa kukubingirisha mpaka juu kabisa kusipo na maji halafu yenyewe yanarudi kwa kasi nasisi tunanyanyuka na kuyafuata tena, jambo moja gumu la kuzingati wakati umapojirusha kwenye wimbi la aina hiyo hutakiwi kuvuta pumzi, Mpaka litakapokuacha. Maji ya chumvi ukiyavuta puani au ukiyanywa kwa wingi wakati unapoogelea ni rahisi sana kukuua.