PICHA: Chukua tahadhari; ukiona hivi usisogelee bahari, ni hatari!

Sijawahi kutamani kuoga baharini,na sasa hivi nimeshazeeka huwa naiangalia kwa mbaali tu kama picha flani hivi...
 
Mimi pia naungana na wewe kama vipi njoo online nikufungee weee mbaka uchoke maana kwenye huo mchezo wa draft naamini nimeshindikana mbaka sasa
 
Wiki hii mwanzoni jirani yetu kapoteza mtoto wa 19 yrs na mjukuu wake wa 5 yrs

Wamezama baharini.. ..

Tahadhari ni muhimu sana!
 
Genta una Ids nyingi
 
Huu mchezo wako kidogo utoe roho lakini kwa style nyingine, sisi tulikuwa tunatembea hadi maji ya kifua then tunaogelea eneo hilo sasa sielewi baharini kukoje maana huku nyuma tulipotoka maji yanajaa wakati eneo tulipo maji yakawaida tu labda yanafikia shingoni. Mzee wakati wa kurudi ndio ikawa kimbembe maji mengi hadi hatuonekani, ikawa ni mwendo wa kuruka juu unapumua then unazama tena huku unasogea taratibu na siku hiyo nikaiaga bahari mazima
 
Maji nayaogopa kinoma, nilishakoswa na ajari mbili za kwenye maji.

Acha niendelee tu kuwa mtazamaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…