Picha: Daktari wa ‘MOI’ muhimbili na nesi wake mbaroni kwa rushwa

Nilishawahi kusema jf imejaa madaktari na madaktari wanafunzi na ndio hao wanamtetea daktari mwenzao. Kila siku mnasema rushwa ma trafic na police.... Sasa huyo dokta anataka milioni
 
Mgonjwa mmoja milioni moja . Je akipata wagonjwa wa 5 au 10 kila mwezi + kwa mwaka + SALARY . NDIO MAANA WANA DHARAU NA WANA UHAKIKA WA KUGOMA NA KUIGOMEA SERIKALI
 
Dah hawa madokta noma.....kichwa MILIONI 1. hata mapolisi, mahakimu etc . Ndio maana wakimaliza chuo tu wana magari na majumba. HIVI HAWA MADOKTA WANA DINI KWELI?
 
hakuna maadili ya kazi na viapo wameweka kando hujikusanyia kipato kisicho halali .yaani hivi sasa mtu akiajiriwa tu muda mfupi anataka atembelee mercedes ,nyumba nzuri ,kutanua matokeo yake ndio haya tunaona hapo juu ,kwanini usisubiri mshahara wako ewe trafiki ,wewe nesi wewe ,afisa ardhi ,na wengineo na tujenge maadili ,huyo unayechukua hela zake yeye pia huzipata kwa shida
 
yaani wewe dada si nakujua wewe ni yule nesi tena umegraduat juzi kati apa,, dah ama kweli sasa unataka kujenga horofa mapema unashindana na walograduate miaka ya 90's au niaje, sor sory kama ni kweli ulihusika pata ilyo haki yako na wee doc,, tena na kitengo kizuri kama hicho afu unakula peupe kiivyo tumia basi akili afu ulidai nyingi afu inaonekana ulidai kwa nguvu mno mpaka wakaamua kukusue in dah,, pole saaana maana nasi tupo kwa thread
 
Tunataka rushwa za tender na mikataba ya kimatafa sio rushwa njaa hizi. Huenda huyu Dr. Anamtoto anamsomesha saint Marys sasa kataitiwa na ada. Hata hivi siungi mkono rushwa hata ya pipi kifua. Takukuru na wenyewe wanatakiwa kuchunguzwa mali zao wamezipata wapi maana wanahela vijana na mali za ukubwa zaidi ya umri wao.
 
that is soo sick...kwa hiyo wasingekua na hiyo hela huyo mgonjwa asingefanyiwa operation ama? hii nchi jamani...too much
 
Kwa ujinga wetu tatizo hili Lina nukuliwa kama ni la hao wahitakiwa wakati ukweli ni kwamba tatizo lililopo ni la mfumo mzima. Pesa ximetolewa kwa majina mbalimbali Kama "Asante" C.C.D N.K na wakati kesi hiyo inaendelea ndugu na wagonjwa wanaendelea kutoa pesa ili kupata huduma.
 
Polisi, immigration, mahakimu, traffic etc..... Wanachukua rushwa elfu 2 , 10 hata laki. Lakini sio milioni tena kwa mgonjwa masikini. Maana angekuwa tajiri angeenda aghakhan, tmj ,kairuki etc
 
doktaz harafu jumapili au ijumaa unaenda msikini au kanisani. Hivi hata moyo haukuumi au kukusuta. Milioni ataitoa wapi mtu yuko hoi kalazwa. Tena tumbi hospital
 
Ajali kazini, ila kwa daktari kudai rushwa ili amhudumie mgonjwa inasikitisha
 
KUANZIA HAO TAKUKURU, POLICE MAHAKIMU NA WENGINE WOTE WALIOHUSIKA Ni Nani ambaye hajawahi kupokea mlungula!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!1 sema tu ni kwa vile ho limesanuka ndo maana twajifanya wasafi. mahakimu wahukumuni hao nayi mjue one day mtahukumiwa maana nanyi mnaokota!!!!
 
Mnaosema rushwa ndogo kumbukeni hizi ndio zinazowaumiza moja kwa moja wananchi....Tuwa challenge Takukuru lakini tusiwaonee huruma hawa dagaa pia japo.... maisha magumu lakini
 
Lakini hawa Takukuru mie binafsi naona waganga njaa tu hata siku moja hawajawahi kumkamata kigogo yoyote zaidi ya kuwaonea mahakimu na watu kama hawa ambao hawana nguvu za kiuchumi.

Mkuu leo unamwaga pwenti kama huna akili nzuri, nimekupa like yangu ya kwanza.
 
Sasa huyo mwenye mgonjwa, baada ya hapo mgonjwa wake alimpeleka wapi kwenda kufanyiwa hiyo operesheni?? Kama wamemuacha afanyiwe haphapo moi madaktari wengine si wanaweza fanya makusudi kwa hasira ya mwenzao kutoswa...!!
 
Sidhani kama watanzania tumetumia hekma ktk suala hili, Tumeweka siasa hata ktk masuala muhimu ya Afya, Sasa masuala ya Epa na Richmond yanahusiana vp na suala la Rushwa hospital?!!! Tulichambue jambo kulingana na wkt wake na umuhimu wake kwa jamii.
 
Hawa TAKUKURU wasitufanye si wajinga wanadhani kukamatisha hivyo visenti vyao kwa watu masikini Kama madaktari na mahakimu ndio tuwaone wanafanya kazi!

Uzandiki mtupu; mafisadi Na wezi wa mabilioni wanawaacha wanadai tuwapelekee orodha wakati wanawajua mafisadi na Wala rushwa.

TAKUKURU wamekwishashindwa na serikali yao dhaifu
 
MMh maskini mgonjwa wa watu,vp sasa hali yake?
 
Nilishawahi kusema jf imejaa madaktari na madaktari wanafunzi na ndio hao wanamtetea daktari mwenzao. Kila siku mnasema rushwa ma trafic na police.... Sasa huyo dokta anataka milioni

Mkuu kupe, nadhani utakuwa umeenda mbali sana(some accusations).

Naomba ni ungane na wewe kusema kuwa kuwa SI SAHIHI(if it will be evident,in this case) kwa daktari kudai/kupokea rushwa kwa ajili ya matibabu.

Lakini kwa upande mwingine nadhani watu (hata JF members) wamekuwa wakitoa rushwa hata bila kuombwa kwa ajili ya matibabu.Na kwa taasisi kama ya MOI hapa, ndio shida, maana hata gharama zake pia ziko juu(and take it from me watu wanatoa rushwa hizo za laki 8 hadi milioni katika hospitali)..ni wagonjwa wachache( wasiotoa rushwa wenyewe au kwa kuombwa) katika hospitali hapa na mikoani pia, pengine ni kutokana na wingi wa wagonjwa,na watu kutaka huduma ya haraka.

Hivyo basi, rushwa(CCD) imekuwa mtindo/tamaduni hospitalini(karibu hospitali zote).
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…