Kila siku katika mabara yote ya dunia wanaongezeka watu wanaofahamu kwamba katika zama zetu hizi, matatizo yanayohusu nia ya kuhimiza maendeleo yanaweza kutanzuliwa kwa sharti la kudumisha amani duniani.
Kukosekana kwa busara katika zile taarifa za serikali ya Marekani kwamba amani ya mataifa inaweza kuhakikishwa kwa nguvu ya silaha za nyuklia, kunazidi kuonekana kwa watu wengi zaidi wenye akili timamu, kati yao wakiwemo watu wenye umri tofauti na kazi tofauti, tena watu wa tabaka mbalimbali wenye kufuata mawazo tofauti ya kisiasa na dini tofauti.
Kwa CCM suala la vita na amani lina maana kubwa kabisa katika maisha ya Watanzania ya kila siku. Ni wazi kabisa Chama cha Mapinduzi kipo kwenye safu ya mbele ya wapinzani wa Vita. Ni wazi kwamba kila Mtanzania hata akiwa na umri gani au digrii gani hubakia kuwa mwana wa Chama tawala ambacho kimemhakikishia uhai, kimempatia msaada alipohitaji na pia kimemhifadhi kutokana na shida zake, maradhi na hatari za kila aina.
Kwa CCM hakuna maafa yaliyo makali zaidi kuliko yale yaliyowapata Watanzania. Na hakuna maumivu makali zaidi kama yale yaliyowapata wananchi wa Tanzania, wala hakuna msiba mkubwa zaidi kuliko kifo cha Mtanzania.
Hapo zamani iliaminiwa kwamba ni viongozi tu ndio wanaoweza kujadili masuala ya usalama. Kwa sasa, lakini, masuala ya usalama yanajadiliwa na mamilioni ya watu ambao hawataki tena kuvumilia kutengwa na shughuli za kuamua matatizo hayo yenye umuhimu mkubwa kwenye maisha yao.
Hali hiyo inachomoza sasa kwenye ngazi ya kitaifa na kwenye medani za kimataifa.
Lakini nafasi ya kuushawishi uamuzi wa masuala ya kisiasa kwa kupitia mabunge na vyombo vingine vya utawala kumbe ni ndogo sana. Ukweli huo unathibitishwa kwa zile shughuli za kusambaza duniani makombora ya Kimarekani, yaani shughuli zinazokubaliwa na serikali za mataifa yanayopokea silaha hizo bila ya kujali lawama za wananchi.
Ndiyo maana CCM lazima ishiriki kwa dhati katika shughuli za kulaumu vikali maandalizi ya vita vya kinyuklia kama ndiyo uharamia mkali kabisa dhidi ya binadamu. Tunaamini kwamba bado inawezekana kuondosha hatari ya maafa ya kinyuklia.