Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Ukienda mjini leo, unaweza kuhisi ni sikukuu au mwisho wa juma (weekend), baada ya barabara kufungwa kutokana na ugeni wa marais na viongozi mbalimbali wanaoshiriki mkutano wa kimataifa wa Nishati unaoanza leo, Januari 27, 2025 jijini Dar es Salaam.
Ilivyozoeleka siku ya Jumatatu katikati ya mji, kuna mishemishe na purukushani za hapa na pale, lakini hali ni tofauti leo, kwani watu si wengi kama ilivyo kawaida, na kimya kimetawala maeneo mbalimbali.
Fuatilia: Mkutano wa Nishati Afrika (Africa Energy Summit) 27-28 Januari, 2025
Baadhi ya maduka yamefungwa, na maeneo kama Kariakoo hakuna msongamano wa magari; hata bajaji ni ngumu kuzipata, ingawa bodaboda wapo wawili watatu.
Hali hii inaweza kudumu kwa siku hizi mbili za mkutano huu, ambao unafanyika Tanzania, ukiwa ni mkutano wa kwanza kuwakutanisha marais zaidi ya 20 kwa mara moja.
Tangazo la Jeshi la Polisi lililotolewa Jumamosi Januari 25, 2025 na Kamanda Kanda Maalumu ya Polisi Dar es Salaam, Jumanne Muliro, lilieleza kuwa kutokana na ugeni wa viongozi watakaokuja kwenye mkutano, barabara zitafungwa.
PICHA: Mwananchi
Soma, Pia
• DAR: Barabara 9 kufungwa kwa siku sita kupisha mkutano wa madini chini ya Viongozi kadhaa wa Afrika