KWELI Picha halisi imetumika kutengeneza video isiyo halisi kwa Akili Unde

KWELI Picha halisi imetumika kutengeneza video isiyo halisi kwa Akili Unde

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Wakuu Hili tukio kwenye video hii ni la kweli?
1757058894251.png

​
 
Tunachokijua
Akili Unde (AI) ni seti ya teknolojia zinazoiwezesha kompyuta kutekeleza majukumu mbalimbali ya kina na kwa uwezo mkubwa kadri ya maelekezo ya mtumiaji, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kuona, kuelewa na kutafsiri lugha inayozungumzwa na maandishi, kuchanganua data, kutengeneza picha na video na kutoa mapendekezo ya utatuzi wa matatizo mbalimbali.

Aidha teknolojia hii imekuwa muhimu katika kurahisisha ufanisi wa shughuli za kila siku na hii ni pindi tu inapotumika kwa nia iliyo njema, lakini inapotumiwa kwa nia ovu huweza kusababisha madhara makubwa kwa watu, mathalani uwepo wa taarifa potofu unachangiwa pia na teknolojia hii ambayo watu hutumia kutengeneza na kusambaza taarifa zisizo sahihi mfano picha, sauti, na video.

Siku za karibuni kumekuwa na ongezeko la maudhui yanayotengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Unde yanayosambazwa mtandaoni hasa picha na video ambayo yamekuwa yakipotosha uhalisia

Mathalani video moja iliyochapishwa katika mtandao wa TikTok ikionesha tukio lisilo la kawaida ambapo inaonekana ndege kubwa inayopaa usawa karibia na watu pamoja na majengo huku watu wakionekana kutishika na hali hiyo.


Je, video hiyo ni halisi?

Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google Reverse image search umebaini picha hali ya eneo hilo ambayo si video ambapo Tovuti ya Habari RDC ilitumia iliitumia picha hiyo Aprili 13, 2020 na kubainisha kuwa eneo hilo linapatikana Bunia, Ituri Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Kwa kutumia nyenzo za kidigitali imebainika kuwa Picha hiyo ambayo ni halisi imetumika kutengeneza video isiyo halisi kupitia teknolojia ya Akili Unde.

Vilevile video hiyo ina mapungufu yanayokinzana na uhalisia jambo linalodhihirisha kuwa imetengenezwa kwa aakili unde. Mathalani baadhi ya watu kuungana miili, kubadilika kwa mavazi ya watu, baadhi ya watu kupotea, pikipiki kugeuka kuwa baiskeli huku matairi yakipotea.
​
1758263386013-png.3475720
Poleni sana waanga wa jambo hilo (kwa sauti ya tesla robot)
 
Kwa macho ya kawaida, kwa akili ya la saba D unagundua kabisa hiyo ni AI
 
Nimecheka sana ndiyo maana mwanamtandao lowasa alisema elimu,elimu,elimu hivi kweli kwa akili ya kawaida unashindwa kabisa kuona watu wanatembea kama mazombi na pikipiki zinageuka zinakuwa baiskeli.
 
Dah alafu ukileta hoja nzuri humu unaambiwa mambo ya IQ ndogo ilihali Kuna hoja humu ni komedi toshaa, akili ya kawaida INATOSHA kabisa kuonyesha ni AI


Deal of million dollars, kwishaaaa
 
Imetokea muda si mrefu,wanaelekea Tukuyu
 
Hii imetokea hapa bonyokwa , mabati ya nyuma nyingi yamefumuka
 
Jata hapa bariadi imepita helkopta ya kijani inapita chini chini inatishia wananchi
 
Back
Top Bottom