PICHA: Hawa ndio waliomuua mwandishi wa Channel Ten (Daudi Mwangosi) huko Iringa



Tukio la Kuuawa Mpiganaja Daud Mwangosi Nyororo - Iringa lilivyotokea​


Tanzania tunakoelekea si kwenyewe, mambo haya sasa lazima kupeleka kwenye vyombo vya usalama na watetezi wa haki za binadamu kimataifa ieleweke hali ya Tanzania ilivyo kuliko tunavyojitokeza kifua mbele kila kukicha kwamba Tanzania tuna amani.
  1. Marehemu Daud Mwangosi anauawa huku ameshikilia video camera na namkoba wake wa vifaa vya kazi ya uanahabari.
  2. Mkuu wa Upelelezi Polisi mwenye shati la light blue na kofia nyeusi kashika pistol akiinyosha hewani.
  3. Kamanda wao mwenye kirungu akiwa katikati akitoa amri ya kuua
  4. Plisi mwenye kofia nyekundu ana pistol
  5. Aliyepewa amri ya kumwua Daud Mwangosi ameshika sila kali ya kivita ya masafa marefu kana kwamba ni kuwindana vita vya msituni.

Napata picha kwa nini nchi nyingi na hasa zilizoendelea ni marufuku polisi kutumia silaha kali za kivita isipokuwa ni silaha za masafa mafupi ambazo ni pistol. Hapa katika tukio kuna waliokuwa na silaha za masafa mafupi ambazo ni pistol zinaonekana wazi, lakini wakaamua kutumia silaha kali ya kivita ya masafa marefu ile watumiayo vita vya nchi kavu na vya msituni.

Kadiri ya wazoefu waliopitia hata somo la jiografia kusoma picha unaona wazi marehemu hakuna na chombo cho chote chenye kuleta madhara kwa polisi, bali ni vifaa vyake vya kazi ambavyo amekufa amevishikilia mkononi na begani ambavyo ni video camera na mkoba wa vifaa vya uandishi.

Kwa tukio hili tunatazamia kusikia utetezi wa jeshi la polisi dhidi ya utumiaji nguvu uliokithiri, kwani morogoro wamechepusha kwa vile tukio halikuwa recorded na vyombo vya habari, lakini hili ni wazi kabisa ambapo taswira zinatoa picha kamili ya kilichojilia.
 
Hivi ni risasi ndio zimeharibu mwili kiasi hiki au ameripuliwa kwa bomu?

Kama ni risasi, mwili ungeharibika kiasi hiki? Kama ni risasi ndio zimeparaganya mwili, ni risasi ngapi zimetumika?

Unajuwa mabomu ya machozi yanavyokuwa discharged?unatafuta loophole ya kuidisqualify hii habari ama hili tukio?maswali gani haya?
 
Kwakweli haya ni mauaji mabaya sana ni dhahiri polisi wana tumika!
 
Unajuwa mabomu ya machozi yanavyokuwa discharged?unatafuta loophole ya kuidisqualify hii habari ama hili tukio?maswali gani haya?

Nimeuliza kama "layman" nataka kufahamishwa. Sina nia ya ku-disqualify au ku-qualify hapa.
Wewe unafikiri ni risasi ndio zimeacha mwili kama unavyoonekana pichani au ni bomu ndio limeharibu mwili hivyo?

Mleta mada, n00b amesema alikuwepo eneo la tukio, pengine anaelewa nini kilitokea. Au yeyote aliyeshuhudia ,atueleze kadhia yenyewe.
 
NAKUUNGA MKONO IGP NA WAZIRI WAKE WONDOKE NDANI YA MASAA 12 HAMNA KISINGIZIO :spy:
 


Pichani Mwandishi Daud Mwangosi akiwa kazini mwenye suruari nyeupe ameshika camera mkononi
 
Nonda angalia hilo bomu limepigwa at close range na sifa ya bomu lazima lilipuke kinachotofautisha makali ya bomu ni umbali, uwezo wa mlipuko na mengineyo. ila hapo wamemlipua mshikaji. hilo ndio jeshi letu la failure
 
hilo ni bomu mkuu,na huwa linakuwa discharged na silaha inayoonekana kama bunduki,ama hujui hiyo kitu?unaona kabisa hapo picha ya kwanza akiwa mikononi mwa polisi na RPC akiwa mzima na camera yake na huyo polisi mmoja akimwelekezea kitu kama bunduki tumboni,tena wakiwa tayari wameshamdhibiti na wengine bastola nje nje!na picha inayofuatia yuko in pieces,sasa hapa polisi wameuwa.Unachotakiwa ni kulaani mauwaji hayo na si kuanza kuleta disputes.You should've understand,ama concern yako ni kitu gani hapa?Kama ilisemekana ni risasi kutokana na silaha aliyoibeba muuwaji huyo,halafu mwili umeonekana tofauti,basi use common sense ujuwe ni bomu lilokuwa discharged,na kama hujui uliza kwa namna ya kutaka kueleweshwa na si kuleta maswali kama ya kukosoa ama kuonyesha kwamba hakuna credibility kwenye reporting.Ni hayo tu kama umeelewa pouwa.
 
Kana kwamba jambo lilikusudiwa, na mtazam wao kwa tukio ni kama wanaashiria wamefanikiwa kumtoa adui wao mkubwa, macho yao yanatoa tafusiri ya wazi mno.

Wanatia hasira hawa jamaa[/QUOTE]



Marehemu Daud Mwangosi akiwa katika moja ya matuko ya wanahabari Iringa akihojiwa na mwanahabari mwenzake maarufu kwa jina la Mzee wa matukio, ndugu Francis Godwin.
 
caught on camera!!!! nawapa pongezi sana waliopiga picha hizi. rpc anasemaje, aijipii anasemaje???
 
waandishi wa habari kwa haya mnayotendewa, kesho na kesho kutwa mkiitwa na kupewa bahasha mjisahaulishe na kuanza kuipamba serikali eeeh


Kwanini waandishi wa habari wasi-susie kutoa/kuandika habari za wizara ya mambo ya ndani mpaka waone hatua zimechukuliwa? Hivi wakisusia ina maana waajiri/mabosi wao watawalazimisha? Mimi nafikiri huu ni wakati muafaka wakuonyesha mshikamano wa; watakao-asi basi ndio kipindi chakujipambanua kujua mbivu na mbichi. Huu ndio wakati muafaka wakujua walio-commit kwenye uandishi na wasindikizaji hasa ni kina nani. Kama kweli una commitment kwenye hii kazi is going to get worse as 2015 approaches. Ni muhimu kujiwekea mikakati sasa. Kwakweli nimesoma comment zote am just speechless.
 
caught on camera!!!! nawapa pongezi sana waliopiga picha hizi. rpc anasemaje, aijipii anasemaje???

Me too...mpiga pich hizi anastaili pongezi kubwa sana.Hakuna haja ya kuunda tume, picha zinajieleza vya kutosha.
 
Haya ndio matunda na ubishi wa chadema. Watanzania wameshajua nia yenu toka mliposema nchi haitatawalika. Mwingine alidiriki kusema eti jk asiende arusha. Kama chadema wangefuata amri ya polisi yote yangetokea?

Shut your mouth, coz ni vizuri kukaa kimya kuliko kuropoka, ina maana umependa polisi hivyo walivyofanya?
 
huyo aliekuwa anaepigwa kikatili sio mwandishi.coz mwandishi dakika 20 kabla ya kuuawa alikuwa kavaa jeans ya blue.huyu jamaa anaepigwa kikatili kavaa kadet ya kaki!
Asante sana kwa kuweka sawa taarifa.
 
jmushi1

Nimesom michango mingi ya thread hii.inasemwa polisi wameua. Picha pia zipo. Pia kuna taarifa za polisi kupiga mabomu kutawanya wananchi. Kwangu mimi haikuwa black and white kujua ni risasi au bomu ndio limetumika katika mauaji haya. Inawezekana mkuu hasira zilizojaa kichwani mwako kimetafsiri maswali yangu kama dispute lakini kwangu mimi ni kutafuta info. kutokana na mwili ulivyoharibika nimepata tabu kufikia hitimisho kuwa ni risasi, na ndio nikatupa masuali yangu.
Ili kukidhi kiu yako, "nalaani vikali unyama/uharamia/mauaji haya yaliyofanywa na wale ambao tunategemea watulinde.

Lakini tusiishie kwenye kulaani tu.Tuhakikishe haki inatendeka. Mwandishi hakuwa na silaha kwa hiyo hakuwa tishio kwa kundi/kigenge cha askari polisi waliomzunguka. Ushahidi unaonesha ni intended murder!
 
Aisee hii nchi inakuwaje? yaani kweli askari anadiriki kulenga mtutu wa bunduki tumboni ilihali yuko sentmita chache tu? jamani hapa ni kumshitaki IGP, RPC na hao askari kwa mauaji yao... maana sasa inaonekana huu mchezo wao umezoeleka
 
Kikosi cha polisi kimegeuka kuwa genge maalum la kuzuia harakati za demokrasia kutambaa nchini. jeshi limekosa ethics, linalindwa na watawala unaojali ubinfasi na kupuuza heshima ya wananchi.

Lazima RPC awajibike, wahusika wote washitakiwe kama sio leo iko siku lazima wasimame kujibu tuhuma za mauaji kama hayo. Sad day in the history of Tanzania. Unapoanza kuuwa wananchi kwa sababu ya kukupinga basi unakosa legitimacy ya kuongoza.

Iko siku watasimama kwenye hukumu ikiwa duniani au akhera kwa mauaji ya kinyama na utumiaji wa excessive force kwa raia wasio na hatia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…