Je, unaweza kutumia nyenzo mbalimbali za kidigitali zinazokuwezesha kuthibitisha uhalisia wa picha?
Mdau, huku ukieleza nyenzo uliyoitumia, bainisha eneo halisi ambapo picha hii ilipigwa.
Mdau, huku ukieleza nyenzo uliyoitumia, bainisha eneo halisi ambapo picha hii ilipigwa.
- Tunachokijua
- Je, wajua? Upotoshaji unaweza kutokea kwa kutumia picha ya zamani au picha ya eneo moja kutumika kuwaaminisha watu kuwa picha hiyo inahusiana na tukio au taarifa husika ambayo huenda ikawa ni ya kupotosha.
Hizi ni baadhi ya nyenzo muhimu za kidigitali ambazo zinakuwezesha kubaini uhalisia wa picha na kuepuka kupotoshwa.
1. Kutumia Google Image Search- Ingia kwenye browser na andika "Google Image Search."
- Apload au paste picha unayotaka kuchunguza.
- Ruhusu Google kuitafuta na angalia matokeo kama picha hiyo inapatikana kwenye vyanzo vingine.
2. TinEye- Nenda kwenye tovuti ya TinyEye.
- Apload au paste URL ya picha unayotaka kuchunguza.
- TinyEye itatafuta picha hiyo au zinazofanana na kuonyesha matokeo.
3. Kurejelea Metadata ya Picha
Metadata ni programu au mfumo unaosaidia kutoa maelezo yanayohusiana na data ya picha, kama vile tarehe ya picha ilipochukuliwa, eneo, na vigezo vingine vya kiufundi.
Unaweza kutumia programu hii ukapata maelezo kama tarehe na eneo zinaweza kutoa mwanga kama picha inaweza kuwa ya zamani au imebadilishwa.
Mfano tunahitaji kufahamu eneo halisi ilipopigwa picha hii tukitumia Google reverse image search.Kupitia Google reverse image search na TinEye inabainisha machapisho mbalimbali yanayohusisha picha hiyo na kueleza mandhari ya kuchomoza kwa jua katika vilima vya matope vilivyopindapinda, mifereji ya mmomonyoko, na mto mkavu katika kituo cha Zabriskie, Hifadhi ya Taifa ya Bonde la Kifo, California, Marekani.