PICHA: Hii ndio stage ya Fiesta Dar es salaam Jumamosi hii

PICHA: Hii ndio stage ya Fiesta Dar es salaam Jumamosi hii

Tangopori

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2012
Posts
1,628
Reaction score
1,285
Hapa bado haijakamilika, ni stage ambayo kukamilika kwake inachukua siku kumi ikiwa inatengenezwa… ni stage ambayo itakua na winch ya kupandisha wasanii kuja kufanya show, kutakua na screen za kisasa zaidi kuonyesha kila kinachoonekana kwenye stage..

Kama unavyoona kwa mbali, kwa mara ya kwanza Fiesta hii backstage yake imejengewa nyumba ya kisasa zaidi na ndefu kwenda juu, ndani yake kutakua na baa, screen kubwa, makochi ya kisasa kwa ajili ya watakaokuwepo hapo.


Hii ni stage nyingine


Ukiangalia kwa makini hapa kuna stage mbili kubwa ambazo zimeunganishwa na barabara ambayo inamuwezesha msanii kutembea juu huku mashabiki wakiwa pembeni kulia na kushoto yani…
Hivyo ni baadhi tu ya vitu nimeamua kukupa kwa sasa mtu wangu, ungana na mimi saa moja usiku kwenye AMPLIFAYA ya Clouds FM ujue mengine mengi kuhusu teknolojia itakayotumika jumamosi hii kwenye stage ya Fiesta Leaders club Dar es salaam.

source



Unaambiwa hii ndio stage ya Fiesta Dar es salaam Jumamosi hii | TZA
 
Kumbe fiesta ni jumamosi hii!!

Mmmmh,haya tamasha jema,... mi nilishasahau kwenda kwenye matamasha ya hawa watu hata aje nani!
 
sijui kitu. stage yenyewe mbona mbaya au kwakua haijakamirika? mia
 
Halafu mwambieni Ruge kuwa show siyo stage. Watu wanataka msanii mkubwa. Mnatumia mahela mengi kutengeneza stage ili eti apande mvuta ndumu Afande Sele. Upuuzi
 
Halafu mwambieni Ruge kuwa show siyo stage. Watu wanataka msanii mkubwa. Mnatumia mahela mengi kutengeneza stage ili eti apande mvuta ndumu Afande Sele. Upuuzi

kule ilboru nilionja cha Arusha kimekaa hadi leo duh hatari by the way mimi nina aleji na mambo yote wanayoandaa CLOUDS media so wafu wataenda wawaone wafu wenzie shit.
 
Fiesta si starehe, kwanza watu hilo nyomi lake nio balaa halaf humo humo kuna waliokosa ustaarab wanakuja kuwaibia wenzao, wanawake wanafanyiwa vitendo sivyo na hata parking sometime ni shida unaweza ukaamua kuondoka then unakuta mtu amekublock njia na hujui atatoka saa ngapi. Acha nishuhudie kwa tv tu.
 
Wanaharibu mazingira tu hapo. Uwanja mzurii utachafuka kwa vinywaji vyenye chemicals na kuua nyasi, matakataka etc. Si mngefanyia club nn sijui ilioandaliwa maarum kwa mambo kama hayo?
 
J martin kila siku yuko Tz me nilijua ni local artist.wajinga ndio waliwao keshaona chimbo tz ndio maana kila cku yuko huku.

eti ndio msanii wa kimatawifa huyo.........aisee siku hizi clouds sijui wanalipeleka wapi hili tamasha
 
Back
Top Bottom