PreGE2025 Picha: Hii ndiyo miradi inayotarajiwa kupitiwa na mwenge wa uhuru, Ruangwa 2025

PreGE2025 Picha: Hii ndiyo miradi inayotarajiwa kupitiwa na mwenge wa uhuru, Ruangwa 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mpepetaji

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2025
Posts
346
Reaction score
213
Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Hassan Ngoma, amefanya ziara ya kukagua na kuhakiki miradi mbalimbali ya maendeleo itakayopitiwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 pamoja na barabara zitakazotumika katika mbio hizo.

Ziara hiyo imefanyika leo Mei 21, 2025, ambapo Ngoma ametembelea maeneo mbalimbali kuanzia Namichiga ambapo Mwenge utapokelewa hadi Nandagala Mwenge utakapokesha.

Akiwa kwenye ziara hiyo, Ngoma ametembelea miradi yote, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule, barabara, visima vya maji, vituo vya afya, na miradi ya vijana na wanawake, ili kuhakikisha maandalizi yote yanakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa kabla ya kupokelewa kwa Mwenge wa Uhuru Mei 28, 2025.

Pia soma: Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze

Miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa shule ya sekondari Namakuku, kituo cha polisi Nandagala, barabara ya Mwilahi, ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) Namakuku, uchimbaji wa visima vya maji, na mradi wa lishe Namichiga, pamoja na miradi ya mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI, rushwa, dawa za kulevya, na ukatili wa kijinsia.

Katika ziara hiyo, Ngoma amewataka watendaji wote wanaohusika na usimamizi na utekelezaji wa miradi hiyo kuongeza kasi ya utekelezaji katika siku chache zilizobaki kabla ya mbio hizo kuwasili. Ameeleza kuwa Mwenge wa Uhuru ni tukio la kitaifa lenye uzito mkubwa, hivyo hakuna nafasi ya uzembe au uzorotaji katika hatua ya maandalizi.

“Miradi hii ni kielelezo cha utekelezaji wa ilani ya serikali na dhamira ya kuwaletea maendeleo wananchi. Tunataka miradi yote iwe imekamilika ipasavyo kabla ya kuwasili kwa Mwenge wa Uhuru. Tuwajibike kikamilifu,” amesema Ngoma.

Kwa mujibu wa ratiba, Wilaya ya Ruangwa itapokea Mwenge wa Uhuru kutoka Manispaa ya Lindi tarehe 28 Mei 2025 katika Uwanja wa Shule ya Msingi Namichiga A, ambapo miradi 17 imepangwa kutembelewa, kuzinduliwa, na kuwekwa mawe ya msingi.

Katika Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu, kauli mbiu inasema “𝐉𝐢𝐭𝐨𝐤𝐞𝐳𝐞 𝐊𝐮𝐬𝐡𝐢𝐫𝐢𝐤𝐢 𝐔𝐜𝐡𝐚𝐠𝐮𝐳𝐢 𝐌𝐤𝐮𝐮 𝐰𝐚 𝐌𝐰𝐚𝐤𝐚 𝟐𝟎𝟐𝟓 𝐤𝐰𝐚 𝐀𝐦𝐚𝐧𝐢 𝐧𝐚 𝐔𝐭𝐮𝐥𝐢𝐯𝐮”
1747904791027.png
1747904819572.png
1747904896216.png
1747904844987.png
 
Mbona vitu vya kawaida sana, mwenge unatakiwa kuzindua vitu vyenye maslahi mapana ya taifa, kituo cha polisi yan tena cha kawaida.
 
Mkuu nitafutie kiwanja Cha makazi hapo Ruangwa Mjini..
 
Back
Top Bottom