Kwa kutumia nyenzo za kidigitali zinazokuwezesha kuthibitisha uhalisia wa picha, bainisha eneo halisi picha hii ilipopigwa na Nyenzo uliyotumia.
- Tunachokijua
- Uhakiki wa Picha kwa kutumia Google Image Search ni njia muhimu ya kubaini asili au maelezo zaidi kuhusu picha fulani.
JamiiCheck imekuandalia utaratibu wa hatua kwa hatua wa jinsi ya kutumia Nyenzo hii kufanya uhakiki wa picha. Rejea kiungo hiki kufuata hatua zote.
Mfano tutumie picha hii inayoonesha makazi ya watu yaliyo karibu na mlima mrefu. Je, ilipigwa wapi na lini?
Uhalisia wa picha
Jamiicheck imejiridhisha kuwa picha hiyo ni halisi. Kwa kutumia Google Reverse Image Search Michael Dr Gumtau alichapisha picha hiyo katika tovuti ya flickr tarehe 20, Novemba 2009 akibainisha ilikuwa ni Mbeya mwaka 1978.
Kadhalika ilichapishwa katika tovuti ya wikimdedia Mwezi Machi 2012, na kuelezwa kuwa ni Mbeya, Tanzania mnamo mwaka 1978.