SI KWELI Picha hii ni mke wa Maduro akiwa amepigwa na wamarekani

SI KWELI Picha hii ni mke wa Maduro akiwa amepigwa na wamarekani

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Hii sio haki hata kidogo, Maduro na mke wake ni waovu yes lakini sio kumtendea hivi.

Imagine Melania angekua amepigwa hivi jee dunia nzima sahizi wangelikua washatoka kusema ni uvunjifu wa haki za wanawake.

Hii sio sawa hata kidogo....

20260107_222322.jpg
20260107_222054.jpg
Screenshot_20260108-105654_X.jpg
Screenshot_20260108-105224_X.jpg
 
Tunachokijua
Januari 03, 2026 Rais wa Marekani, Donald Trump, alitangaza kuwa Marekani ilifanya mashambulizi makubwa ya kijeshi dhidi ya Venezuela na kufanikiwa kumkamata Rais wa nchi hiyo, Nicolás Maduro, pamoja na mke wake.

Inaelezwa kuwa tangu Nicolás Maduro achukue hatamu za uongozi mwaka 2013, Venezuela imepitia misukosuko mikubwa ya kisiasa na kijamii ambayo imesababisha shutuma nzito za ukiukwaji wa haki za binadamu ambapo mashirika ya kimataifa yamekuwa yakiandika ripoti mbalimbali zinazoonyesha mbinu za kimfumo zinazotumiwa na Serikali kudhibiti upinzani na kukandamiza uhuru wa raia.

Januari 05, 2025, Maduro, na mke wake Cilia Flores, walifikishwa kwa mara ya kwanza katika mahakama ya shirikisho ya Manhattan baada ya kukamatwa na majeshi ya Marekani.


Madai

Kumekuwapo na picha inayosambazwa mtandaoni ikidaiwa kuwa ni mke wa Cilia Flores akiwa mahakamani ambaye anayeonekana akiwa ameumizwa jicho lake la kushoto.

Je, picha hiyo ni halisi? ina uhusiano wowote na mke wa Maduro?

Kwa kutumia nyenzo za kidigitali JamiiCheck imejiridhisha kuwa picha hiyo si halisi kwani imebainika kuwa na viashiria vya akili unde katika sehemu ya uso jambo linaloonesha kuhusika kwa teknolojia hiyo kutengeneza picha husika.​
screenshot-2026-01-09-101048-png.3527326

Kadhalika picha hiyo haifanani na muonekano halisi wa Cilia Flores mke wa Maduro. Rejea rangi ya nywele ambayo haifanani nywele za Cilia. Kadhalika rejea hereni pande zote mbili ambapo hazifanani jambo ambalo si la kawaida katika picha halisi.​

Rejea hapa muonekano wa Cilia Flores.
cilia-flores.jpg

​
Kwa mujibu tovuti ya ABC News wakili wa Cilia Flores alimweleza jaji wa shirikisho wa Marekani kwamba Cilia alipata majeraha makubwa wakati wa kukamatwa kwake nchini Venezuela.

Akizungumza na jaji wa shirikisho anayesimamia kesi yake ya jinai, wakili wa Flores, Mark Donnelly, alimwambia Jaji Mkuu wa Mahakama ya Wilaya ya Marekani, Alvin Hellerstein, kwamba mteja wake alipata majeraha makubwa wakati wa kutekwa kwake, na akaashiria kuwa huenda alipata mfupa kuvunjika au michubuko mikubwa katika mbavu zake, na kwamba anahitaji uchunguzi wa kimwili wa kitabibu.​
Kwa kuwa simfahamu mke wa Maduro, nimefanya AI query na imeleta majibu haya:

Picha hiyo uliyopost inatumiwa sana kwa sasa kwenye mitandao ya kijamii kimakosa. Hiyo ni picha ya mwanamke wa Australia anaitwa Rebecca Howe. Alipata majeraha hayo mwaka 2022 wakati wa tamasha la bendi ya Guns N' Roses. Mwimbaji Axl Rose alitupa maikrofoni (microphone) kwa mashabiki na ikampiga Rebecca usoni.

Picha hii inahusishwa na Cilia Flores (mke wa Nicolás Maduro) ambaye alikamatwa na kufikishwa mahakamani New York akiwa na majeraha usoni na bandeji baada ya operesheni ya kijeshi nchini Venezuela.

Watu kwenye mitandao wanatumia picha ya Rebecca Howe (kutokana na kufanana kwa majeraha ya usoni) kudai kuwa ni Cilia Flores baada ya kukamatwa. Huu ni upotoshaji wa picha (misinformation).
 
Hiyo inaitwa ' Humiliation ritual' , ya secret societies.

Viongozi wengi na watu maarufu kuna nyakati wamepitia hiyo. Utakumbuka karibuni hata Musk alikuwa nayo hiyo alionekana akiwa White House
 
Back
Top Bottom