- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
- Tunachokijua
- Mara baada ya uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mkuu 2025 uliofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Agosti 28, 2025 Kawe jijini Dar es Salaam chama hicho kiliendelea na kampeni zake mkoani Morogoro Agosti 29 hadi Agosti 30.
Kumekupo na Picha inayosambazwa mtandaoni ikionesha idadi kubwa ya watu waliobebwa na malori huku wakiwa na bendera za kijani na kudaiwa kuwa imepigwa katika kampeni za CCM mkoani Morogoro, Agosti 2025.
Je, ni kweli picha hiyo ni ya Agosti, 2025?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google reverse image search umejiridhisha kuwa picha si ya mwaka 2025 kama inavyodaiwa, kwani imebainika picha hiyo iliwahi kuchapishwa mtandaoni Septemba 12, 2015.
Hivyo matumizi ya picha hiyo kurejelea kampeni za uchaguzi mkuu 2025, ni kupotosha uhalisia.
Rejea kiungo hiki kuona picha nyingine zilizoambatana na picha hiyo mwaka 2015.