- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Wakuu
====
'Picha imepigwa 1995 pale Zambia Mama Betty Kaunda alijua kupendeza kuliko uyo kibungo Wako' mwenye ukweli wa hizi taarifa naomba msaada.
====
'Picha imepigwa 1995 pale Zambia Mama Betty Kaunda alijua kupendeza kuliko uyo kibungo Wako' mwenye ukweli wa hizi taarifa naomba msaada.
- Tunachokijua
- Madai
Kumekuwepo na Taarifa zinazoambatana na picha ya mdada akiwa juu ya gari na kudaiwa kuwa ni picha ya mke wa aliyekuwa Rais wa Zambia, Beatrice kaunda (Betty) mwaka 1955.
Mtumiaji mmoja wa mtandao wa X aliambatanisha na ujumbe kuwa;
“Picha hii imepigwa pale Zambia Mama Betty Kaunda alijua kupendeza kuliko uyo kiubungo wako”
Uhalisia wa madai hayo
Baada ya ufuatiliaji wa kina wa jamiiCheck, imejiridhisha kuwa pichani si Betty kaunda.
Utafutaji kwa kupitia google reverse Image search unabainisha kuwa picha hiyo imepigwa miaka ya 1970 na mwandishi wa habari picha kutokea nchini Ghana. Mpiga picha huyo anafahamika kwa jina la James Barnor.
Ufuatiliaji zaidi umebainisha kuwa picha hiyo inajulikana kwa jina la Woman posing on James Barnor's car, Accra, c.1970. Tovuti ya Sotheby inaeleza kuwa;
“Baada ya kuhamia Uingereza, Barnor alirudi Ghana na kuanza kupiga picha za watu mitaani badala ya kwenye studio yake. Kazi hii ya sanaa inaonesha kuwa ni ya miaka ya 1970, wanawake wa Ghana walikuwa wakikumbatia mitindo ya nywele asilia, huenda wakichochewa na fahari ya baada ya uhuru na harakati za ufahamu wa Weusi zilizokuwa Marekani. Mkao wa mhusika unaashiria uhuru—si tu kutoka katika ukoloni au ubaguzi wa rangi, bali pia uhuru mpya wa wanawake.”
Aidha kuonesha kuwa picha hiyo ni ya nchini Ghana miaka ya 1970, tazama hapa kuona picha nyingine iliyopigwa na James, miaka hiyo katika gari hilo hilo likiwa na namba zile zile za usajali yaani “GR 4506”