- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Mdau anauliza 'Kwanini tukifika hapa lazima mahubiri yaanze?'' je, hapa ni wapi?
- Tunachokijua
Uhakiki wa Picha kwa kutumia Google Image Search ni njia muhimu ya kubaini asili au maelezo zaidi kuhusu picha fulani.
JamiiCheck imekuandalia utaratibu wa hatua kwa hatua wa jinsi ya kutumia Nyenzo hii kufanya uhakiki wa picha. Rejea kiungo hiki kufuata hatua zote.
Mfano tutumie picha hii inayoonesha barabara iliyopita katika mlima mrefu ikiwa na kona kali. Je, ilipigwa wapi na lini?
Uhalisia wa picha
Jamiicheck imejiridhisha kuwa picha hiyo ni halisi.
Hata hivyo picha si ya Tanzania, rejea mistari ya pembeni ya barabara yenye rangi nyeupe ambayo ni tofauti na Tanzania ambayo ni ya rangi ya njano.
Kwa kutumia Google Reverse Image Search imebainika picha hiyo imechapishwa na vyanzo mbalimbali mtandaoni vinavyoeleza kuwa ni kutoka nchini India. Tovuti ya WordPress ilichapisha picha hiyo mwezi agosti 29, 2009 na kwamba ni
barabara ya Mumbai–Goa karibu na mlima wa Kashedi.