- Tunachokijua
- Uhakiki wa Picha kwa kutumia Google Image Search ni njia muhimu ya kubaini asili au maelezo zaidi kuhusu picha fulani.
JamiiCheck imekuandalia utaratibu wa hatua kwa hatua wa jinsi ya kutumia Nyenzo hii kufanya uhakiki wa picha. Rejea kiungo hiki kufuata hatua zote.
Mfano tutumie picha hii inayoonesha mandhari ya milima ambapo inaonesha gari na watu waliopo kwenye barabara iliyopo juu mlimani sehemu inayoonekana kuwa hatari. Je, ilipigwa wapi na lini? ina uhusiano wowote na Tanzania?
Uhalisia wa picha
Jamiicheck imejiridhisha kuwa picha hiyo ni halisi. Kwa kutumia Google Reverse Image Search imebaini picha hiyo iliwahi kuchapishwa mwaka katika tovuti ya Flickr na Roberto ambapo alibainisha kuwa ni barabara ya kifo iliyopo nchini Bolivia.
Hivyo picha hiyo hiyo si kutoka Tanzania.
Kupitia Google earth inaonesha muonekano wa picha katika eneo hilo nchini Bolivia.