- Source #1
- View Source #1
Mitandaoni kumeibuka mjadala kuhusu muonekano wa msanii wa Tanzania, Juma Jux, baada ya baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii kudai kuwa msanii huyo amepungua uzito kwa kiasi kikubwa. Baadhi ya machapisho yameambatana na picha na video zake za hivi karibuni, huku watumiaji wakijiuliza iwapo mabadiliko hayo ya mwonekano yanaashiria kuwa Jux ana tatizo la kiafya.
- Tunachokijua
- Juma Musa Mkambala (JUX) ni msanii wa Tanzania anaejulikana zaidi kwenye R&B/Bongo flava pia ni mwanamitindo na ana brand yake inayoitwa African Boy, Pia kwenye upande wa mahusiano Jux ameoa binti wa Nigeria Priscilla Ojo na ana mtoto mmoja wa kiume anaitwa Rakeem na aliwahi kuwa kwenye mahusiano na msanii mwenzie wa Bongo Flava Vanessa Mdee lakini hawakufunga Ndoa.
Madai
Kumekuwepo na picha zinazosambaa mtandaoni hususani kwenye mtandao wa X zikiwa na maelezo mafupi yanayosomeka “Asiye funzwa na VANESA atafunzwa na Prissila” huku picha hizo zikimuonyesha Jux akiwa amepungua mwili tofauti na hapo awali wakati akimuoa Priscilla.
Uhalisia wa madai hayo
Baada ya ufatiliaji wa kidigitali wa kubaini maudhui yaliyo tengenezwa na akili unde (AI) imebainika kuwa picha halisi zimechapishwa kwenye ukurasa wa instagram wa jux akiwa katika harusi ya TikToker Peller nchini Nigeria pamoja na mkewe na kuhaririwa kwenye akili unde (AI) hali iliyopelekea picha hizo zipoteze uhalisia wake na kuzua taharuki mtandaoni.