- Source #1
- View Source #1
Naomba kuwa na uhakika picha iliyotolewa na millard naona itakuwa ya akili unde.
- Tunachokijua
- Rais wa Finland Alexander Stubb alifanya ziara yake nchini Tanzania Mei 14 hadi Mei 16, 2025. Akiwa Tanzania alipokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na baadaye kutembelea maeneo mbalimbali.
Kuanzia Mei 16, 2025 zilisambaa picha kutoka kwa watu mbalimbali wakioneskkana kupiga picha na Rais huyo wa Finland. Miongoni mwa waliochapisha picha wakiwa na Rais Stubb ni mwandishi wa habari Millard Ayo. Tazama hapa.
Uhalisa wa picha hiyo
JamiiCheck imefuatilia picha hiyo na kubaini kuwa ni halisi. Ufuatiliaji umebaini kuwa Rais wa Finland Alexander Stubb alipiga picha na watu mbalimbali siku hiyo ya Mei 16, 2025 katika eneo hilo linaloonekana pichani.
Miongoni mwa watu waliopiga picha na Rais Alexander Stubb ni mtangazaji Frida Amani ambaye aliipost picha hiyo Mei 16, 2025. Mtumiaji mwingine wa mtandao wa X, @JuliMuhindi alichapisha taarifa iliyoambatana na picha akiwa amesiamama na Rais Stubb Katika eneo lile lile.
Aidha ufuatiliaji kwa kutumia nyenzo za kubaini picha zilizotengenezwa kw akutumia akili unde (AI) zimebainisha kuwa picha hiyo ni halisi. Nyenzo ya Sight engine imebainisha kuwa picha hiyo ni halisi kwa 99%.
Nyenzo ya Huggingface pia imebainisha kuwa kuna uwezekano mkubwa wa picha hiyo kuwa halisi kuliko kutengenezwa kwa Akili unde (AI).
Matokeo ya nyenzo ya Sight engine
Matokeo ya nyenzo ya hugging face