SI KWELI Picha hii ya Netanyahu akishangaa mavazi ya mwakilishi wa New Papua Guinea ni halisi?

SI KWELI Picha hii ya Netanyahu akishangaa mavazi ya mwakilishi wa New Papua Guinea ni halisi?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Je huyu ni Rais wa New Papua Guinea ambaye Waziri mkuu wa Israel anamshangaa kutokana na mavazi yake?

1790681203294.png
1790681171950.png
 
Tunachokijua
Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kumekuwa na picha inyaosambaa ikimuonesha Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akimsangaa mwanaume mmoja kutokana na mavazi ya asili aliyoyavaa. Picha hiyo inadaiwa kuwa imechukuliwa katika mkutano wa mkuu wa Umoja wa Mataifa (UNGA), 2026.

Ufuatiliaji kwa kutumia zana za kidigitali umebaini kuwa picha hiyo imehaririwa kwa kutumia zana za kidigitali ili kupotosha. Picha halisi ilichukuliwa mwaka 2017 ambapo mwanaume huyo aliyekuwa kwenye mavazi yake ya asili alikuwa ni mkumbe kutoka New Papua Guinea.

Mwanaume huyo anafahamika kama Ngalum Uropkulin ambaye alihudhuria makao makuu ya Umoja wa mataifa katika mkutano kuhusu masuala ya utamaduni. Mwanaume huyo si Waziri Mkuu wala Rais wa New papua Guinea kama ilivyodaiwa na vyanzo mbalimbali kwani pia taifa hilo halina Rais.

Hitimisho; Picha inayomuonesha Netanyahu na Ngalum imehaririwa kwa kutumia zana za kidigitali kwa kumuongeza Netanyahu katika picha hiyo kwa lengo la kupotosha.
Kwa kutumia ufuatiliji wa Google Reverse Image Search umebaini kuwa picha hiyo haimuoneshi Rais wa Papua New Guinea. Badala yake, inaonyesha kiongozi kutoka Papua New Guinea aliyeshiriki katika jukwaa la Umoja wa Mataifa

Ufuatiliaji zaidi umebainisha kuwa mjumbe huyo alkuwa anaitwa , Ngalum Uropkulin,ambaye alihudhulia umoja wa mataifa mnamo mwaka 2017 na akiwa na mavazi ya jadi

Licha ya hivyo Pembe hiyo, inayojulikana kama koteka, hutumiwa na makabila ya magharibi mwa Papua New Guinea katika maisha ya kila siku na katika shughuli mbalimbali za maisha yao ya kila siku.
Katika hatua nyingine, imebainika kuwa picha ya Waziri Mkuu wa Israel benjamin netanyau iliyowekwa katika picha hiyo imehaririwa kwa kutumia teknolojia ya akili unde .
 
Back
Top Bottom