- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Wakuu huko mitandaoni inasambaa picha ya Rais William Rutto na kudaiwa kuwa amevaa mashati ya Marehemu Wicknell Chivayo.
Je ni halisi?
Je ni halisi?
- Tunachokijua
- William Ruto ni mwanasiasa ambaye ni Rais wa Kenya. Amewahi pia kushika nafasi ya Umakamu wa Rais wa Taifa hilo wakati wa utawala wa Rais Uhuru Kenyatta.
Wicknell Chivayo alikuwa ni mfanyabiashara kutoka nchini Zimbabwe aliyejijengea umaarufu mkubwa miongoni mwa watu wengi barani Afrika kutokana na ukaribu wake na baadhi ya viongozi wa mataifa barani humo. Chivayo alifariki Oktoba 1, 2026 kwa ajali ya Helkopa akiwa na mkewe.
Miongoni mwa Marais aliokuwa na ukaribu nao ni Rais wa kenya, William Ruto ambapo wameonekana mara kadhaa wakiwa pamoja huku mara ya mwisho walionekana wakiwa pamoja katika sherehe ya mtoto wa Ruto iliyofanyika nchini Kenya.
Madai
Kupitia kwenye mitandao ya kijamii kuanzia Oktoba 21, 2026 kumeibuka picha inayosambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo X (Tazama hapa) na Facebook (tazama hapa) ikimuonesha Rais Ruto akiwa amevalia shati kubwa zaidi na kudaiwa kuwa ni la Wicknell Chivayo.
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefuatilia kwa kutumia zana za kidigitali ikiwemo reverse image search na kujirirdhisha kua picha hiyo imehaririwa kwa kutumia zana za kidigitali na hivyo kupotosha. Picha hiyo imehahariwa kutoka katika picha halisi iliyochapishwa mtandaoni kutokana na tukio la Oktoba 16, 206 wakati Rais William Ruto alipokuwa akizundua soko la Masinde Muliro, katika Kaunti ya Trans Nzoia.