Kupitia mitandao mingi ya kijamii kumekuwepo na picha zinazosambaa kumuonesha aliyekuwa Rais wa Kenya Uhuru Kenyata akiwa na ishara inayoelezwa kuwa ni ya Freemason. Mtumiaji mmoja wa
mtandao wa X alichapisha;
"The shirt has a logo of freemason and also a tattoo on his arm. We are rules by a class of cultists"
Uhalisa wa Picha hiyo ni upi?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa picha hiyo si halisi bali imehaririwa kwa kutumia nyenzo za kidigitali.
Kwa kutumia nyenzo ya google reverse image search imebainika pia picha hiyo ni kutoka katika
miongoni mwa picha alizopiga Uhuru Kenyatta February, 2023 alipokuwa nchini Nigeria.
Kenyatta alkuwa nchini Nigeria kama kiongozi wa waangalizi chini ya Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Afrika.
Ufuatiliaji zaidi umebaini kuwa alama zinazoonekana zimepachikwa kwa kutumia Nyenzo za kidigitali kufuatia kukosa uhusiano wa moja kwa moja na shati hilo na kuashiria kabisa zimepachikwa tu.
Aidha katika picha zake nyingine ambazo Kenyatta amekuwa akivaa nguo za mikono mifupi hajawahi kuonekana kuwa na ishara ama alama (tatto) mkononi mwake kama ilivyodaiwa kwenye picha hiyo.