View attachment 3149286
View attachment 3149299
Hatimaye PPP ya David Kafulila iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria namba 103 ya mwaka 2010 ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2014, 2018 na 2023 yaanza kuzaa matunda kwa Watanzania hasa baada ya kuanza kutumia marekebisho mapya ya Sheria hiyo ya mwaka 2023.
PPP kwa kumtumia mbia mzawa toka kampuni ya Tosh Logistics Limited watajenga jengo kubwa zaidi ya lile la Mlimani City lenye thamani ya TZS 36.7bn wakati matumizi yatagharimu kiasi cha TZS 13.3bn litakalokuwa na wapangaji zaidi ya 900 lenye ghorofa 10 kwenda juu.
Mkurugenzi Mtendaji wa PPP-Centre Bw. David Kafulila ameiambia kamati ya Bunge ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kuwa Dar es Salaam City Council's Economic and Development Corporation (DDC) katika wakati wote wa Ujenzi wa mradi huo kila mwaka watajizolea kiasi cha TZS 2 bilioni na baada ya mradi huo kukamilika watalipwa kiasi cha TZS 2.5 bilioni kama kodi ya jengo tu bila kuhesabu kodi na shuru mbalimbali na baada ya muda wa mkataba jengo hilo litakuwa ni mali halali ya serikali ya Tanzania.
Mkurugenzi huyo ameiambia kamati hiyo ya Bunge kuwa Ujenzi wa mradi huo ni miongoni mwamiradi yenye mikataba bora zaidi ya uwekezaji kuwahi kushuhudiwa hapa kwenye ardhi ya Tanzania.
Mkurugenzi huyo ameipongeza kamati hiyo ya Bunge huku akiomba ushirikiano kati ya TAMISEMI na PPP ili kwa pamoja waweze kuvuta mitaji toka sekta binafsi ili kujenga miradi yenye tija kwa Taifa ambayo itatupatia Kodi na tozo mbalimbali na hivyo kuchochea ukuaji wa Uchumi wetu huku Serikali ikiachwa ifanye miradi ile tu ambayo haina sura ya kibiashara na hivyo kuipa nafuu zaidi Serikali katika kutafuta Mikopo na misaada mbalimbali toka kwa wahisani.