Ugonjwa unaweza kuwa Ni Discoid Eczema/Discoid Dermatitis au Taenea Corporis..
Habari Daktari Mambo.
Ushauri wako muhim nisaidie.
Nikienda kuishi miji ya baridi (mfano nilipoenda shule Arusha mwaka 2010 na sasa nipo Cape Town) nasumbuliwa sana na tatizo la mwili kuchoma choma.
inatokeaje?
- Mfano nikianza kukimbia jogging mwili ukaanza kupata joto, ama nikatoka home mchana nikaanza kutembea jua likanipiga mwili ukaanza kuchemka... Naanza kuchomwa chomwa sana over my "upper body" kuanzia kifuani hadi kichwani.
- pia nikiwa nervous, mfano natakiwa nifanye presentation mbele ya watu, ile anxiety feeling naanza kuchomwa chomwa sana usoni, shingoni.
Feeling nayokua napata ni kama vile mtu ananichoma choma na sindano mwilini (upper body). Nakua natamani nipate maji nijimwagie pengine nitapoa.
Lakin nikishatulia tu, basi inapoa.
Nisaidie hivi itakua tatizo gani.
Nime Fanya research wanaita "Winter Itch Attack"
Nitumie dawa gani kupona.
Mbona nikirudi Dar / sehem isio na baridi simpati hili tatizo?
Sipati upele, vibarango wala makovu.... Ni mwili unakua unachoma choma tu. Hata nikijikuna haisaidii.. hadi mwili upoe wenyewe.